![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgUQeDwRaaY4DTSdBBskEQcegoIJpfUlpnxKseWnSurJqfWEik604-LjnFuObpvRShRcyB1Fu-CUoUCS9KkWfW0dnUYTjO5qv5mm1SY23NNADRcaXAg2dP9kOE6Sf1QF3_2KMGYM9gXqqI/s200/product_thumbnail.jpg)
Huu ni mwongozo wangu wa pili kuuchapishwa, baada ya Notes on Acebe's Things Fall Apart, mwongozo ambao umekuwa ukitumiwa na wanafunzi na waalimu wa fasihi sehemu mbali mbali duniani kama nilivyowahi kugusia katika blogu hii.
Kila mwongozo unaongelea kazi tajwa lakini pia unagusia kazi zingine za fasihi ili kupanua uwanja wa ufahamu juu ya fasihi. Kila mwongozo unaingiza pia vipengele vya nadharia ya fasihi vinavyohusika katika kazi inayojadiliwa. Kwa hiyo, kwa kusoma mwongozo moja, mtu anajifunza au anapata fursa ya kutafakri mambo mengi.
Nina nia ya kuandika miongozo mingine ya kazi muhimu za fasihi ya Afrika. Unaweza kujipatia mwongozo huu mpya na vitabu vyangu vingine katika duka la mtandaoni
No comments:
Post a Comment