
Ukiona jembe limechakaa, ujue linatumika. Kitabu hiki ni sawa na jembe. Mashuhuda ni waMarekani wenye shughuli yoyote na waAfrika, pia waAfrika kama Abraham Thomas wenye shughhuli yoyote na waMarekani. Kinaepusha migogoro na kuchangia ufanisi.

Mjasiriamali wa Arusha anauza kitabu hiki ambacho kimekuwa gumzo huku nje ya Tanzania hadi hivi karibuni katika Trade With Africa Business Summit, mkutano uliohudhuriwa na watu maarufu kutoka nchi mbali kuanzia Umoja wa Afrika, hadi Israel, Ujerumani, Nigeria, Ghana, Afrika Kusini, na Marekani. Piga simu namba 0787 597 202
Sijawahi kufika Mwitongo, Butiama, lakini kitabu changu, ambacho ni kama nafsi yangu, kimefika. Pichani anaonekana mjukuu wa Mwalimu Nyerere akiwa anasoma kitabu hiki. Picha hii aliiweka mitandaoni akiwa ameambatisha ujumbe. Ninanukuu baadhi ya aliyosema.Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...