Monday, October 24, 2022
Mdau Amechapisha Mapitio ya Kitabu Changu
Saturday, October 1, 2022
Nimekutana na Wasomaji Wangu
Sarah na mimi tumefahamiana tangu Julai 2019, aliponikuta kwenye maonesho ya vitabu mjini Blaine, Minnesota, akaipatia kitabu cha "Africans and Americans: Embracing Cultural Differences."
Baadaye Sarah alichapisha kitabu cha mashairi yake kiitwacho "Vita, Babel, Cauliflower," ambacho nilikisoma nikakifurahia, na kisha nikakiandikia uhakiki. Unaweza kuona kisehemu cha uhakiki wangu kwenye tovuti ya Amazon. Sarah ana kipaji kikubwa cha utunzi wa mashairi ya kiIngereza.
Katika maongezi yetu ya leo, nimefahamu kuwa baada ya kusoma kitabu changu cha "Africans and Americans: Embracing Cultural Differences," Sarah alianza kumwelezea rafiki yake wa miaka mingi Brighid juu yangu na kitabu hiki..
Kutokana na hayo, Brighid alifurahi sana kukutana nami leo. Alikuwa na nakala ya kitabu, kikiwa kimepigiwa mistari kwenye vifungu na sentensi nyingi, kuashiria kuwa amekuwa akisoma kwa uangalifu na tafakuri tele. Nilishangaa anavyokumbuka hata mambo madogo yaliyomo kitabuni.
Tuliongea kwa masaa matatu, na muda mwingi tuliongelea tofauti za tanmadunni nilizozielezea kitabuni. Lakini pia tuliongelea uwezekano wa kushirikiana katika utatuzi wa mahitaji mbali mbali katika jamii za Afrika Mashariki, kama vile elimu na maji. Tumefurahi kugundua kuwa wote tayari tumekuwa tukifanya hayo. Brighid, kwa mfano amekuwa akifanya shughuli hizi Arusha. Tumehamasika kufanya zaidi.
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, ambayo ni tarehe 17 Agosti, 1951. Familia yangu, ndugu, na marafiki wamejumuika nami kushereh...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasih...