Friday, April 2, 2010

Wenzetu Wanazindua iPad, Sisi Tunazindua Bia

Mapema leo niliandika ujumbe mdogo kwenye ukumbi wa Tanzanet, ambao ni ukumbi wa mijadala, taarifa, na michapo unaowajumuisha waTanzania na marafiki wa Tanzania duniani kote. Ujumbe wangu unahusu mambo mawili tofauti, ambayo yanatokea wiki hii: moja ni uzinduzi wa kifaa kiitwacho iPad, na jingine ni uzinduzi wa bia kule Tanzania.

Muda mfupi baada ya kutokea ujumbe wangu kule Tanzanet, nimeandikiwa na wahusika wa blogu ya Watanzania waishio Oslo kuwa wanapenda kuiweka makala yangu kwenye blogu yao. Nami sikuwa na kipingamizi. Bofya hapa.

8 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

safi saana ndo maisha yetu, na bado bia za kampeni za uchaguzimkuu

Evarist Chahali said...

Inasikitisha sana.Ni yaleyale ya watoto wa wenzetu kuchezea kompyuta ilhali sie wanachezea vifuu kama sio kombolela.

Albert Kissima said...

Tanzania tuna safari ndeeeeeefu ambayo kwa bahati nzuri tuna kila chenye umuhimu kwa safari hiyo ila kwa bahati mbaya sana safari hiyo hatujaianza. Itaanza pale tu tutakapopata wazalendo wa kutuongoza. Tutakuwa tumechelewa ila itabidi tujiaminishe kuwa hatujachelewa na haraka tuianze safari.

Mbele said...

Katika suala la malezi ya watoto, inaonekana wa-Tanzania tumeamua kuwa ulabu ni muhimu kwa watoto wetu.Bofya hapa

Subi Nukta said...

Prof, katika siku ambazo umenichekesha basi nileo. Yaani baada ya kusoma kichwa cha habari nimeangua kicheko cha ghafla.
Kamala, naungana nawe 100% mwaka huu wa uchaguzi lazima watu wabebwe kwa toroli.
@Evaris, Albert, Prof na Namala, asanteni kwa kuchangamsha akili yangu leo.
You guys are just great!

Mbele said...

Dada Subi, nami nilivunjika mbavu niliposoma michango ya wadau hapa juu. Nilitaka nimwambie Kamala kuwa najiandaa kuja Tanzania, kuwahi hizi bia za kampeni :-)

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

karibu prof. pendine mbali na bia waweza ambulia hata 'boda boda' (pikipiki ya kampeni....lol

Mbele said...

Ndio siku za kwenda Bongo zinasogea. Sijui nikaanzie na bia za chama kipi.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...