Kitabu Kinapopigwa Marufuku

Kati ya mambo yanayosumbua sana akili yangu ni kitabu kupigwa marufuku. Sijui kama wewe unaafiki kupigwa marufuku kwa kitabu chochote.

Katika historia ya vitabu, ambayo ni karne nyingi, vitabu vingi vimepigwa marufuku sehemu mbali mbali za dunia, kwa sababu mbali mbali. Vingi vinaendelea kupigwa marufuku.

Tafakari matukio mawili ya kupigwa marufuku vitabu ambayo yametokea Tanzania. Kitabu kimoja ni Satanic Verses cha Salman Rushdie. Kuna watu waliona ni lazima kipigwe marufuku. Kingine ni Mwembechai Killings cha Dr. Hamza Njozi. Nacho kuna watu waliona ni lazima kipigwe marufuku.

Mtazamo wangu kuhusu suala hili nimeuelezea katika kitabu changu cha CHANGAMOTO, ambacho ni cha uchochezi. Labda nacho kitapigwa marufuku.

Comments

Tabaka au taasisi fulani inapojihisi kwamba imeshambuliwa - na ikajikuta haina uwezo wa kujibu hoja basi inakimbilia kupiga marufuku kitabu. Inashangaza.

Siku hizi za mtandao kidogo ni vigumu kukipiga kitabu marufuku na hiyo marufuku ikafanya kazi kwa asilimia zote. Kwa mfano hiki cha Mwembechai killings unaweza kukinakilisha chote (tena bure) au unaweza kukisoma mtandaoni.
Unknown said…
Haswaaa Masangu.

Profesa, ni vyema kufahamu ni wapi hicho kitabu chako ulichoandika kiitwacho CHANGAMOTO kinapatikana.

Tafadhali, maana ili ikitokea wakakipga marufuku kama ulivyosema tuwe tumeshakisoma.

Chonde chonde!!!
Mbele said…
Suala hili lina mengi. Moja ni kuwa utamaduni wa kununua na kusoma vitabu umefifia katika jamii ya wa-Tanzania. Yaani wa-Tanzania wenyewe wamevipiga marufuku vitabu katika maisha yao.

Sasa kitendawili ni pale anapojitokeza tena mtu, katika nchi hii hii, na kukipiga marufuku kitabu kama kilivyopigwa marufuku kitabu cha Salman Rushdie na kile cha Hamza Njozi.

Ndugu Mcharia, nilipoongelea kitabu changu kupigwa marufuku, kwa kiasi fulani nilikuwa natania. Isipokuwa, nikizingatia hayo niliyosema hapa juu, ni kwamba kitabu hiki nacho hakina nafasi katika jamii ya wa-Tanzania, ambamo vitabu vimepigwa marufuku.

Hata hivi, kitabu changu hiki, na vingine nilivyoandika, kinapatikana Dar es Salaam, simu namba 0754 888 647 au 0717 413 073.

Popular posts from this blog

Kumbukumbu ya Kuzaliwa

Tenzi Tatu za Kale

Pesa za Majini