SUPER MUHOGO: Unga Safi wa Muhogo

Katika pita pita zangu, nimeona tangazo kwenye blogu ya Lady JayDee la wajasiriamali wa Chanika, Dar es Salaam, wanaouza unga wa muhogo. Wamemwomba Lady JayDee awawekee tangazo hilo kwenye blogu yake, naye amefanya hivyo.

Nimevutiwa na jambo hili. Njia madhubuti ya kujenga uchumi wa nchi yetu ni kuzalisha bidhaa na kuziuza nje, ili tupate fedha za kigeni. Kuuza bidhaa zetu nje kunaleta ajira nchini.

Hili ni jambo rahisi kulielewa. Hata mimi ambaye sikusomea somo la uchumi nimeandika kuhusu suala hili katika kitabu changu cha CHANGAMOTO, nikielezea namna mbali mbali jinsi wa-Tanzania tunavyohujumu uchumi wa nchi yetu. Mfano moja ni jinsi tunavyozishabikia bidhaa za kutoka nchi za nje, bila kutambua kuwa tunawapa ajira watu wa nchi zingine. Wakati huo huo, wa-Tanzania wanalalamikia uhaba wa ajira nchini. Tunapaswa kuuza bidhaa na huduma kwa wengine.

Kutokana na yote hayo, nimevutiwa na hao wajasiriamali wanaouza unga wa muhogo. Nimeamua kusaidia kutangaza biashara yao hapa kwenye blogu yangu. Nawatakia mafanikio tele katika kuboresha maisha yao na kuinua uchumi wa nchi.

Comments

Simon Kitururu said…
Yani nafagilia kweli pointi yako hii Prof.


Itabidi niige kwenye blogu yangu au ukiruhusu nitaiposti post yako hiihii Mkuu Prof .J. MBELE!:-(
umenena ya ukweli kabisa wa-Tanzania hawapendi vyao wanapenda vya nje tu. Unga wa muhogo!! nimekumbuka mbali sana umefanya vizuri nadhani ni kweli inabidi nami niweke maisha na mafanikio kwani bla huu unga wa muhogo sidhani ningekuwa mimi leo:-)
Mbele said…
Hapo mmenena. Huu unga ni moto wa kuotea mbali. Unastahili kuanikwa kwenye blogu zenu :-)

Kwenye kitabu changu, nimeongelea jinsi wenzetu wa Nigeria, Ghana, na kadhalika huku ughaibuni wanavyoendesha viduka ambamo wanauza vitu kama unga kutoka kwao, samaki, pili pili, nguo, na kadhalika.

Hapa Marekani, utatukuta wa-Tanzania tunamiminika kwenye maduka hayo. Hata mchele tunanunua katika maduka ya watu wa Thailand, China, Malaysia, na kadhalika.

Tungepaswa tuwe tunauza mchele wa Mbarali. Lakini hatuelewi hata hilo jambo dogo, kwa sababu shule tulitoroka umande ;-)

Hata serikali yetu nayo ilitoroka umande, maana imewahi kutoa ahadi nzito kuwa inatuletea ajira milioni ngapi sijui. Hii ni hadithi ya kusisimua, maana hata hizo ajira chache zilizopo nchini naona wa-Kenya wanakuja na kujichukulia, kwa sababu wao hawakutoroka umande :-)
Unknown said…
Pro J.Mbele tunakushukuru kwa kutuwekea tangazo hili la unga wetu.Wadau wote tunawakaribisha mpate radha ya chakula asilia.
Tunaomba radhi upande wa email inayoonekana kwenye mfuko kuna makosa kidogo inatakiwa isomeke jbocko2010@gmail.com tunataraji kwenye mifuko mipya tutafanya marekebisho haya pia.Aksanteni
Mtesuka said…
umenena vyema Prof. katika masoko ya ushindani, mazao ya kilimo ndiyo yanatupa "competitive advantage".
hansom said…
Nimeipenda bidhaa hii,hongera jorambocko na wenzie,naamini hata prof. Mbelle nae mtamtumia huko Marekani alipo akumbuke nyumbani.
Nami naiweka habari hii katika blogu yangu ili kuwaunga mkono wajasiriamali hawa.
Mbele said…
Ndugu Hansom,

Ni jambo jema kuwaunga mkono wananchi wenzetu na kuwa na mshikamano sisi sote. Maisha yetu wa-Tanzania na wa-Afrika kwa ujumla yamejengeka kimahusiano, katika familia, ukoo, kijiji, na kadhalika.

Popular posts from this blog

Kumbukumbu ya Kuzaliwa

Tenzi Tatu za Kale

Pesa za Majini