Thursday, April 19, 2012

Nimesafiri Salama; Namshukuru Mungu

Nimesafiri salama kutoka Dar es Salaam hadi, nikawasili hapa Minnesota usiku wa tarehe 16 Aprili. Hapa kushoto ni picha niliyopiga ya bawa la ndege ya Swiss Air niliyosafiria. Niliipiga juu ya bahari ya Atlantic.

Namshukuru Mungu kwa kunifikisha salama, nikizingatia kuwa hata kuja kwangu kufundisha hapa haikuwa mpango wangu. Kwa kweli, wahusika walipoanza kuniulizia kama nitakuwa tayari kuja kufundisha hapa, nilisita, sikukubali. Nilikuwa tayari nafundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, baada ya kuishi Marekani miaka ya 1980-86 nikiwa nasomea shahada za juu. Yaliyotokea baada ya hapo, hadi nikakubali kuja kufundisha, ni hadithi ndefu. Nitakapoisimulia, walimwengu watakubaliana nami kuwa ilikuwa ni mpango wa Mungu. Kwa hivi, namshukuru kwa kunifikisha tena salama, niendelee na majukumu aliyonipangia.

9 comments:

emuthree said...

Profesa mbele,mungu akuzidishie heri, maana unachofanya ni hazina kwako na kwa vizazi vijavyo. Tupo pamoja

Mbele said...

Shukrani. Wa-Islam husema, "Allahu Akbar," yaani Mungu ndiye mkubwa na mwenye uwezo kuliko wote. Ni dhana muhimu kuzingatiwa.

Yasinta Ngonyani said...

Nami nasema nami nashukuru umesafiri salama na nakutakia kila la kheri na majukumu yako ya kujenga Taifa.

Anonymous said...

pole na safari kwahiyo hayo chini ya ubawa wa ndege ni mawingu au nimaji ya bahari ya atlantic?

Mbele said...

Ndugu anonymous, shukrani kwa ulizo lako. Yale yanayoonekana chini ni mawingu, ambayo ukiwa hapa duniani unayaona kule juu angani. Ndege inaruka juu kabisa ya yale mawingu, na juu ya hiyo ndege hakuna tena mawingu, bali ni ombwe tu kama unavyoona. Inatisha, na ndio maana binafsi nasema namshukuru Mungu ninapofika salama.

Anonymous said...

mhh kweli asante sana kwa kunielimisha ubarikiwe sana mimi nilifikiri hiyo ni bahari

Egidio Ndabagoye said...

Profesa,
Nitafurahi kama ukituhadithia hiyo safari yako aliokupangia Mungu.

Mbele said...

Ndugu Ndabagoye, shukrani kwa ulizo lako. Nililisoma siku ile ile ulipoandika, ila niliona ni gumu kulijibu, nikawa natafakari.

Ni suala la imani yangu, nikizingatia mkondo wa maisha yangu, tangu kabla sijaanza shule, ambapo nilisikia katika dhamini yangu Mungu akiniita niende katika ualimu. Nilisikia huu wito na nikalenga maisha yangu katika njia hiyo, bila kutetereka, hadi leo.

Kuja kwangu kufundisha Marekani, nikitokea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambapo nilikuwa nafundisha, ni habari ndefu, ambayo naiona ilipangwa na Mungu. Tukipata fursa ya kukutana, nitaweza kukueleza kirefu.

Ndio maana nimediriki kusema kuwa kusafiri kwangu hadi nikawasili salama mahali ninapofanyia kazi ni maongozi ya Mungu.

Huenda wengine wataniona mtu wa ajabu kwa kuamini hivyo, lakini hii ndio imani inayoniongoza katika shughuli zangu. Narudia kutoa shukrani kwa ulizo lako, na shukrani kwa kutembelea hapa kijiweni pangu. Karibu sana.

Tiba asili said...

Kwa wenye shida mbalimbali kama Kusafisha nyota, kumvuta mpenzi aliye mbali, kumtuliza mpenzi wako, n.k nipigie 0742162843


Pia katika katika kipindi hiki cha kampeni kama unahitaji mvuto kuweza kupata uongozi Karibu Pete zipo pia dawa zipo nipigie Simu husitume SMS kuhepuka matapeli.


PIA KWA UHITAJI WAMALI,UTAJIRI AU FEDHA ZA NDAGU AU MAJINI KWA MUDA MFUPI MPAKA MASAA 72(SIKU 3) PAPO HAPO KWA MASHARTI MAALUM KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......



KUMBUKA MALIPO NI BAADA YA KUFANIKIWA



kwa maelezo kamili piga namba +255742162843



(KWANINI USUMBUKE,HACHA KUTANGATANGA, NA MAISHA NI MAFUPI PUUZA UONGOFU WA KUWA MTU KUWA TAJIRI NI DHAMBI WAKATI AKUAMBIAE YEYE NI TAJIRI (Tumia ufahamu kujinasuaUTAJIRI WA NDAGU(MASHARTI) NDANI YA MASAA 72(SIKU TATU) PAPO HAPO KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......



NAITWA DR, MDIRO piga 0742162843. KAMA UNAITAJI PESA ZA MAJINI AU NDAGU YA MALI AU ULINZI KWA MALI YAKO

(HUSITUME SMS PIGA SIMU KUHEPUKA MATAPELI)

MATIBABU MENGINEYO NI KAMA UTULIVU KATIKA NDOA, AU KUMVUTA UMPENDAE, KUONDOA MIKOSI, MABALAA, KUOSHA NYOTA, KUITAMBUA NYOTA YAKO NA ASILI YA KAZI YAKE, KAMA UNASUMBULIWA NA MAJINI MAHABA NA SHIDA YA UZAZI.



NIPIGIE 0742162843. KIKUBWA NI KUSIKILIZA NA KUFATA MASHARTI. ANGALIZO USITUME SMS PIGA NA UWE NA NIA.



(kuhusu utajiri au pesa) KABLA YA KUPIGA SIMU ZINGATIA YAFUATAYO

1. uwe una umri wa miaka 18+

2. uwe tayari kupokea masharti yote

3.uwe na uwezo wa kutunza siri

4. uwe jasiri wa kupokea taarifa yoyote

KARIBU SANA KWA SHIDA NYINGINE PIA ULIYONAYO AMBAYO SIJATAJA INSHAALAH ITATATULIWA IKIWA NDANI YA UWEZO WANGU

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...