Kanisa Lilivyoungua Zanzibar

Kati ya uharibifu uliofanyika Zanzibar wakati wa vurugu za hivi karibuni makanisa yalichomwa moto. Hapa kushoto ni picha ya kanisa likiungua. Nimeipata hapa. Kutokana na kauli mbali mbali mtandaoni, ni wazi kuwa wako watu ambao wamefurahishwa na uchomaji moto wa haya makanisa, pamoja na vitabu vilivyokuwemo humo, kuanzia vya sala hadi Biblia. Wako ambao wanasema kuwa Zanzibar ni nchi ya ki-Islam na u-Kristo hautakiwi kule. Kwa maana hiyo, kuchoma moto makanisa ni kuwakomoa wa-Kristo.

Maajabu ya dunia hayaishii hapa, kwani wako pia watu ambao wanauchukia u-Islam na wanataka kuwakomoa wa-Islam. Wangeikaribisha fursa ya kuichoma moto misikiti. Miezi kadhaa iliyopita, tulipata taarifa za kikundi cha wa-Marekani waliotangaza kuwa watachoma moto Quran. Kabla ya hapo, tulisikia kwamba kule kwenye jela ya Guantanamo, kulikuwa na kitendo cha kuikojolea Quran. Bila shaka, lengo ni kuwakomoa wa-Islam.

Wenzetu ndio hao. Kweli, dunia ina mambo.


Comments

tz biashara said…
Tunatakiwa tuwe huru kimawazo bila ya kuelemea upande mmoja.Na tuwe makini katika kusoma habari za waandishi wetu kwasababu wao ndio wenye kutugonganisha vichwa vyetu.Serikali yetu inasikitisha na kufanya dhulma nyingi mpaka inafikia wananchi kukasirika na kutaka kuondoa muungano labda wameona hakuna faida yoyote ila umasikini unaongezeka hivo wajitawale wenyewe na kuleta ajira pamoja na maendeleo ktk nchi yao.Sidhani kama kweli Wazanzibari hawapendi wakristo kwasababu wapo na wameishi nao miaka mingi japo idadi ni ndogo.Tatizo kubwa ni muungano wenyewe jinsi unavoendeshwa na vilevile kinachowaudhi wazanzibari ni kauli kutoka kwa baadhi ya viongozi wa huku kwetu na kuita Zanzibar ni mkoa na sio nchi.Wanadai kwamba ni dharau kwasababu kama sio nchi kwanini washerehekee sikukuu ya muungano?Na vilevile wachunguze huyu anaehusika na uchomaji wa makanisa yote kwani ni kosa kubwa ktk dini ya kiisilamu kuchoma nyumba za ibada hata kama sio msikiti.Na ni uvunjifu wa amani kwasababu hawa Polisi wetu wanapenda kutumia nguvu wakati akili wanayo.Nilimsikiliza Sheikh Farid akisema kwanini waende wakamchukue shekhe kama wanamteka nyara na hali ya kuwa kila wanapoitwa kwa kosa lolote huwaandikia barua ya kutaka wajisalimishe Polisi na hutimiza kila wanachoambiwa hata kama ni kwenda mahakamani.Sasa iweje leo wanavamia sehamu na kumkamata mtu bila ya kuambiwa kosa lake?Kama unakumbuka wakati wa Mkapa alipeleka jeshi Unguja na Pemba na walifanya maafa makubwa sana.Wamewabaka watoto wa kipemba na wengine wameuliwa na wengine walipotea lakini hakuna repoti yoyote iliyotolewa.Waunguja walipigwa hadharani mpaka leo zipo baadhi ya video ktk youtube.Haya yote hawawezi kuyasahau na ndio kinachowashinikiza kuwa wakijitawala wenyewe angalau kuwepo na human right.Kwakweli wanatutia aibu kwasababu wote ni watanzania na tukionekana kama na sisi ni wanyanyasaji kwakweli ni aibu sana.
Anonymous said…
Waandishi wanatakiwa kua makini sana wanapoandika au kueka picha zao katika taarifa muhimu hasa taarifa kama hizi.
kwamfano muandishi hii picha alioieka sio ya zanzibar wala sio kanisa la zanzibar. huu ni uchochezi mkubwa sana unaofanywa na muandishi huyu. zanzibar kwa kukuhakikishia hasa hakuna kanisa kama hili wala hakuna kanisa ambalo liliungua kama hivi.

Popular posts from this blog

Kumbukumbu ya Kuzaliwa

Tenzi Tatu za Kale

Pesa za Majini