Tuesday, January 1, 2013

Nimeibukia YouTube na Tangazo la Kitabu

Leo, siku ya kwanza ya Mwaka Mpya, nimetua YouTube na kuweka tangazo la kitabu changu kimojawapo, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences. Binti yangu Zawadi ndiye aliyerekodi ujumbe wangu, akaiweka video YouTube. Nimejfunza kutoka kwake.
 

4 comments:

PBF Rungwe Pilot Project said...

Heri ya Mwaka Mpya 2013 Profesa. Nimefurahi kupata maelezo ya kitabu chako kwa njia ya YouTube. Nami nimepata sasa shauku ya kupata nakala ya kitabu chako.
Nakutakia baraka za Mwaka Mpya wa 2013

Unknown said...

Hongera Prof kwa kuibukia You Tube. Tunapaswa kuzitumia fursa za teknolojia kueneza habari njema.

Yasinta Ngonyani said...

Nimefurahi ulivyoamua kufanya yaani kukutangaza kitabu hiki kwa njia hii ya You Tube...

Mbele said...

Wadau, asanteni kwa kauli zenu.

Mdau PBF Rungwe Pilot Project, nina hakika kuwa ukikipata kitabu hiki utakipenda na kitafungua macho kwenye suala hili la kuwaelewa wa-Marekani (na labda watu wa Ulaya pia, ila mimi nawafahamu zaidi waMarekani, na nimewaongelea wao).

Nasema hivyo kwa vile ndio ninayoambiwa na wasomaji. Wasomaji hao ni wa-Afrika wanaoishi Marekani au wenye mahusiano na wa-Marekani. Wa-Marekani wanaohusiana na wa-Afrika au wanaosafiria Afrika nao wanakifurahia kitabu hiki. Ingekuwa nimeamua hivyo, ningekuwa naleta taarifa za watu hao karibu kila wiki hapa kwenye blogu yangu, kwani nazipata daima.

Unaweza kukipata kitabu hiki Dar es Salaam, simu namba 0754 888 647 au 0717 413 073.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...