Friday, February 1, 2013

Nimeleta Wanafunzi Tanzania

Nimekuwa kimya kwa karibu mwezi mmoja. Kisa? Nilileta wanafunzi Tanzania, kutoka Chuo cha St. Olaf ambapo nafundisha. Niliwaleta wanafunzi hao ili kuwafundisha kozi ambayo niliitunga, kumhusu mwandishi maarufu Ernest Hemingway, ambaye alisafiri na kuishi hapa Afrika Mashariki, hasa Kenya na Tanganyika, mwaka 1933-34 na 1953-54.

Tulifika Tanzania tarehe 3 Januari, tukapitia maeneo kadhaa aliyopitia mwandishi huyu hapa nchini petu, tukisoma maandishi yake kuhusu safari zake na matukio mbali mbali sehemu hizo. Maandishi hayo ni riwaya, hadithi fupi, insha, na barua.

Ingawa kazi hii ni nzito, yenye vipengele vingi, nina uzoefu nayo. Nilishaendesha kozi ya aina hii siku zilizopita, kwa wanafunzi wa Chuo cha Colorado, kama nilivyoelezea hapa

Hapo pichani wanaonekana wanafunzi niliowaleta mwaka huu. Ilikuwa ni jioni ya tarehe 28 January, wakati nilipowafikisha uwanja wa ndege wa Kilimanjaro, tayari kwa safari ya Marekani. Insha Allah nitaweka picha na maelezo mbali mbali katika blogu hii.

No comments:

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...