Saturday, February 2, 2013

Arusha: Nimekutana na Mbunge Godbless Lema

Jana, nilienda kujipatia chakula cha mchana sehemu fulani hapa Arusha. Baada ya kuketi, jamaa niliyetanguzana naye alinikonyeza niangalie meza ya kushoto kwangu. Kulikuwa na watu yapata watao, na nilipoangalia zaidi nilimwona Mheshimiwa Godbless Lema, mbunge wa Arusha kwa tiketi ya CHADEMA. Sikuwa nimewahi kumwona kabla, ila sura yake ni ile ile ninayoiona mitandaoni.

Nilifurahi. Nilisimama nikaenda kumsalimia. Nilimwambia "pole na majukumu" na nikamtajia jina langu. Nilimwambia pia kuwa mbunge mwenzake wa CHADEMA, Profesa Kulikoyela Kahigi, ni rafiki yangu wa tangu tuliposoma dara moja Mkwawa High School.

Sikumsalimia kwa vile ni Godbless Lema, bali kwa vile ni mwakilishi wa Arusha. Nilikuwa natoa heshima kwa wapiga kura wa Arusha.

Wakati anaondoka, na watu wake, Mbunge alisogea nilipokaa, akaniaga. Nami nilimweleza kuwa mimi si mwanachama wa CHADEMA, bali ninaunga mkono harakati za CHADEMA za kulikwamu Taifa hili ambalo CCM imelizamisha katika ufisadi. Nilimwambia kuwa tuko pamoja kwa hilo.

1 comment:

Unknown said...

Mhmhmh,,,, Kwa kweli nami nafurahi kwa uamuzi wako wa busara.
Nimefurahi kwa kuwa hukumsalimia ka Mhe. Lema, ilihali wewe sisi mwana-CHADEMA, na kujitamkia waziwazi kuwa unaunga mkono harakati za.... kitu ambacho nami naunga mkono kwa nguvu zote.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...