Saturday, February 2, 2013

Nimekutana na Mdau Wangu Mkubwa wa Arusha

Juzi, tarehe 31, nilikutana na Mama Linda, mMarekani anayishi Arusha. Ni mdau mkubwa wa kitabu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences. Niliwahi kumtaja hapa
Mama huyu tumefahamiana kwa miaka mingi kidogo, na tumekuwa na kukutana Arusha na pia Marekani, anapotembelea kule. Tuna mawazo yanayofanana kuhusu umuhimu wa watu kuzitafakari tofauti za tamaduni, ili kuboresha mahusiano yao.

Yeye ni mshauri wa jumuia ya wageni, hasa wa-Marekani hapa Arusha, kama vile mimi ninavyofanya kwa wa-Marekani na wa-Afrika kule Marekani. Tangu nilipochapisha kitabu changu, Mama huyu amekuwa akikitumia na kukipigia debe. Namheshimu kama mmoja wa wadau wangu wakubwa.

Kila tunapokutana, inakuwa ni furaha sana kwetu, na tunabadilishana mawazo na uzoefu. Kwa miezi kadhaa tumekuwa tukitafakari wazo la kuendesha warsha hapa Arusha kuhusu masuala haya ya tofauti za tamaduni. Tunapangia kufanya hivyo nitakapokuja tena Tanzania.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Inapendeza sana Hongera kukutana maana naona mtakuwa na mengi ya kubadilishana tena..

Unknown said...

Maisha yako yanatupa darasa maridhawa kuhusu kujifunza. Kwamba safari ya kujifunza haina ukomo mpaka itapotamatishwa na kaburi!(Ipo pia imani kwamba kujifunza kunaendelea baada ya umauti).
Baadhi ya watu wanapofikia viwango vya juu vya kielimu, huifanya hiyo kuwa fursa ya kujivika umahiri wa kila kitu na kutowasikiliza wengine. Nashukuru kwamba unatupa mtazamo tofauti. Kila unapopita unajichanganya na watu wa kila kada. Bila shaka unafanya hivi kama sehemu ya KUJIFUNZA na KUWAFUNDISHA wengine. Na kwa kweli, mimi ni miongoni mwa wanaojifunza kutokana na mtindo wako wa maisha!

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...