Nilifurahi nilipoziona picha alizopiga, ingawa yeye si mzoefu. Ninaonekana katika hizi picha zote. Katika picha mbili, mto wa Cannon, ambao umefurika, unaonekana pia.
Nimezileta picha hizi ili kuwathibitishia ndugu na marafiki kuwa hali ya afya yangu inaendelea kuwa njema, ingawa imechukua miezi mingi sasa. Ninategemea kuanza kufundisha tena wakati muhula mpya wa shule utakapoanza, wiki ya kwanza ya mwezi Septemba, Insha'Allah.
Hapa kushoto naonekana nimeketi sehemu ya "park" hapa mjini. Nimeshika mkongojo ambao umenisaidia kutembea kwa miezi kadhaa, ila sasa naweza kutembea bila kuutumia.Nimetoka mbali; namshukuru Mungu.
2 comments:
Pole sana Prof.
Asante sana. Nilikuwa nimekongoroka kweli, ila sasa afadhali. Namshukuru Muumba.
Kila tunapoamka tukiwa wazima na afya nzuri, tushukuru, kwani sio haki yetu. Tutumie fursa hii kwa manufaa ya wanadamu. Ndilo jambo ambalo nimejifunza, baada ya afya kukongoroka kwa miezi, nikashindwa kufanya shughuli nilizozizoea, kama vile kusoma, kufundisha, na kuandika.
Post a Comment