Hapa niko katika baa mojak kwenye mji mdogo wa Longido. Ilikuwa ni mwezi Januari, 2013, wakati nilipokuwa Tanzania nikiendesha kozi ya "Hemingway in East Africa." Naonekana nikisoma kitabu kimoja cha Hemingway, True at First Light.
Nadhani tulikuwa na kipindi baadaye mchana ule, nami nilikuwa katika maandalizi.
Watanzania wengi tumejiaminisha kuwa katika hali ya uchovu na joto, bia ndio wakati wake. Tunasema "kazi na dawa." Sijui kama ni ukweli au tumejiwekea hiyo dhana kwa maslahi yetu tu, au ni uzembe. Labda soda ingetosha, au maji. Sijui.
No comments:
Post a Comment