Saturday, May 13, 2017

Msikilize Raia wa Marekani Anavyomrarua Kiongozi

Jambo moja linalonivutia kuhusu Marekani ni uhuru wa kujieleza. Katiba ya Marekani inalinda uhuru huo kikamilifu. Kwa mfano, kulikuwa na kesi dhidi ya mtu aliyechoma moto bendera ya Taifa, lakini mahakama kuu iliamua na imeendelea kusisitiza kuwa kuchoma moto bendera ya Taifa ni sehemu ya uhuru wa kujieleza, ambao unalindwa na katiba. Mahakama kuu inasisitiza kuwa kauli tata, za kukera, au za kuwakosoa watawala ndizo hasa katiba ilikusudiwa kuzilinda.

Serikali ya Marekani inafahamu kuwa raia ana uhuru na haki kamili ya kuikosoa. Viongozi wa Marekani wanajua hilo. Ninaleta video hapa, inayomwonyesha mwananchi akimfokea kiongozi bila kumung'unya maneno. Mwone kiongozi huyu kutoka chama tawala cha Rais Donald Trump alivyonywea, wakati kipigo kinaendelea.

2 comments:

Anonymous said...

Inatia hamasa, ingekuwa tanzania angekuwa ameshatekwa.

Mbele said...

Ndugu Anonymous, hapa Marekani, hali ndio hiyo. Maadam huyu jamaa anaongea tu, haki yake ya kuongea inatambuliwa na kulindwa. Kama angekurupuka na ngumi au kitu kingine akielekea kumdhuru huyu kiongozi, polisi na wanausalama wanamdaka na kumwondoa hapo ndani. Kazi ya polisi na wanausalama katika mikusanyiko hii ni kulinda amani na uhuru wa watu kujieleza, si kuwazuia watu kusema watakacho.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...