Majungu Kuhusu Nyerere: Jishindie Dola 100

Mengi wanayosema na kuyaamini wa-Tanzania kumhusu Mwalimu Nyerere ni majungu. Hayo nimeyafahamu kwa muda mrefu. Ni wajibu wetu kuandika habari sahihi kuhusu Mwalimu Nyerere kama ilivyo kwa masuala mengine yoyote. Nami, kwa kuanzia, nimechapisha kitabu kiitwacho CHANGAMOTO, ambamo, pamoja na mengine yote, kuna makala na dondoo mbali mbali kuhusu Mwalimu Nyerere.

Kati ya majungu ambayo yanavuma sana ni kwamba Mwalimu Nyerere hatimaye alikiri kuwa Ujamaa umeshindwa. Madai haya yanasikika vijiweni, na nimewahi kuyaona kwenye maandishi pia, kama vile blogu, na gazeti la An Nuur, ambamo kauli alizozitoa Mwalimu Nyerere katika mahojiano na CNN zimenukuliwa, lakini sio kwa usahihi.

Ninavyojua, Mwalimu Nyerere hakuwahi kusema kuwa Ujamaa umeshindwa. Ninajiamini kabisa kwa hilo. Napenda kutangaza kuwa yeyote atakayeleta ushahidi kuthibitisha kuwa Mwalimu Nyerere alikiri kuwa Ujamaa umeshindwa aulete ushahidi huu hapa kwenye blogu yangu. Ikidhihirika kuwa ushahidi umetolewa, nitampelekea mhusika dola 100 kama kifuta jasho na shukrani yangu, kwani atakuwa amenielimisha kwa jambo ambalo sikulijua. Ninathamini sana elimu.

Tangu nilipoanzisha blogu hii, nilitamka kuwa shughuli yake mojawapo itakuwa ni kumwenzi Mwalimu Nyerere. Kuyaanika hadharani majungu dhidi ya Mwalimu Nyerere ni sehemu ya kazi hiyo. Naanza na majungu niliyoyataja hapa juu. Kazi kwenu.

Comments

Anonymous said…
nyerere alitamka hivyo sikumbuki kama alikuwa anongea na waandishi wa habari lakini alisema nilisoma gazeti la nipashe kabla ya uchaguzi wa awamu ya mwisho ya mkapa kuwa ujamaa umeshindwa kama ambavyo ukiristo umeshindwana ndivyo ujamaa ulivyoshindwa.
Kazi kwelikweli,Profesa.Mwalimu Nyerere amakuwa na maandishi mengi,na amesema mambo mengi kuhusu Azimio la Arusha na ujamaa na kujitagemea.
Kwa hiyo kutokana na Home work uliyowapa wana - Blogger watazamia kutafuta wapi na lini kama ni kitabu gani Mwalimu Nyerere alipotamka ujamaa umeshindwa.Huwenda ukampata mtu aliyeshuhudia usemi huo,ili isiwe majungu,bali ni kweli.
Simon Kitururu said…
Lakini kwani UJAMAA haujashindwa?:-(
Anonymous said…
Hata kama tukikubali kuwa ujamaa ulishindwa, huo ubepari wenyewe uliofanikiwa uko wapi? Kwani mnadhani mabepari ni nyie? Au hamuoni sawasawa?
Simon Kitururu said…
@Anony: Kwani UBEPARI umeshishindwa?

Na kama UJAMAA na UBEPARI hakuna kilichofanikiwa,...
.... ni nini kilifanya walioanzisha UJAMAA na UBEPARI tusiwe nao leo hii wakaanzisha ndude nyingine?

Nimeongea kwakuwa nimehisi ANONY umenilenga mie kwenye ndude hii!:-(
Anonymous said…
Nyerere mbona ameshindwa sana kwa nini aliamua kungw'atuka, amekuwa mdini amewabagua waislam hali ya kuwa ndio walio mfanya afikie hapo kama unabisha muulize mzee John Rupia atakupa habari zake vizuri. pili kama si baba wa kanisa iweje muda mfupi tu baada ya kustaafu kanisa limtangaze mwenye heri. msitudanganye bwana zamza za ujinga sasa zimekwisha.
mambo said…
nina mashaka na rekodi za mtoa maoni wa kwanza "kabla ya uchaguzi wa awamu ya mwisho ya mkapa"
Nyerere alifariki 1999, awamu ya kwanza ya mkapa!!!!
Fadhy Mtanga said…
Awali ya yote, naomba nikushukuru sana Prof Mbele kwa kulileta hili.

Ninaitamani sana hiyo dola 100 maana kwa hili giza hapa Bongo, hapana shaka ningenunua mafuta ya taa na mishumaa ya kutosha.

Tuache hayo.

Naomba niseme kwa thabiti na yakini kuwa hapana pahala Mwalimu Nyerere alitamka kuwa ujamaa umeshindwa. Mwalimu simu zote hadi anapatwa umauti alitetea kile alichokiamini, ambacho ni ujamaa.

Mwalimu alipata kusema, alipenda kutembea na vitabu viwili. Biblia na Azimio la Arusha. Anasema amesoma na kurudia tena na tena lakini hakuona makosa katika misingi ya Azimio la Arusha, ambalo lilikuwa na misingi ya ubinadamu na usawa. Mwalimu alisema hivyo kwa kinywa chake.

Mie ni msomaji mzuri sana wa vitabu alivyoviandika Mwalimu. Hakuna pahala amesema hivyo. Nitalisimamia hilo daima. Nimebahatika pia kusoma vitabu vingi vilivyoandikwa na waandishi wengine kuhusu Mwalimu vikiwamo vile vinavyomkosoa.

Hivi karibuni mitandao ya kijamii kama Jamii Forums nayo imekuwa ikiandika mengi sana ya kumkosoa Mwalimu.

Pamoja na udhaifu wowote aliowahi kuwa nao kama binadamu, Mwalimu atabaki kuwa kiongozi wa kipekee ambaye hapajaondokea kuwapo katika Tanzania na pengine asiondokee katika kipindi cha hivi karibuni.

Viongozi wa sasa wanaliona Azimio la Arusha kama sumu kali kwa kuwa hawawezi kamwe kuenenda njia itakiwayo nalo Azimio la Arusha.

Ahsante.ele kwa kulileta hili.

Ninaitamani sana hiyo dola 100 maana kwa hili giza hapa Bongo, hapana shaka ningenunua mafuta ya taa na mishumaa ya kutosha.

Tuache hayo.

Naomba niseme kwa thabiti na yakini kuwa hapana pahala Mwalimu Nyerere alitamka kuwa ujamaa umeshindwa. Mwalimu simu zote hadi anapatwa umauti alitetea kile alichokiamini, ambacho ni ujamaa.

Mwalimu alipata kusema, alipenda kutembea na vitabu viwili. Biblia na Azimio la Arusha. Anasema amesoma na kurudia tena na tena lakini hakuona makosa katika misingi ya Azimio la Arusha, ambalo lilikuwa na misingi ya ubinadamu na usawa. Mwalimu alisema hivyo kwa kinywa chake.

Mie ni msomaji mzuri sana wa vitabu alivyoviandika Mwalimu. Hakuna pahala amesema hivyo. Nitalisimamia hilo daima. Nimebahatika pia kusoma vitabu vingi vilivyoandikwa na waandishi wengine kuhusu Mwalimu vikiwamo vile vinavyomkosoa.

Hivi karibuni mitandao ya kijamii kama Jamii Forums nayo imekuwa ikiandika mengi sana ya kumkosoa Mwalimu.

Pamoja na udhaifu wowote aliowahi kuwa nao kama binadamu, Mwalimu atabaki kuwa kiongozi wa kipekee ambaye hapajaondokea kuwapo katika Tanzania na pengine asiondokee katika kipindi cha hivi karibuni.

Viongozi wa sasa wanaliona Azimio la Arusha kama sumu kali kwa kuwa hawawezi kamwe kuenenda njia itakiwayo nalo Azimio la Arusha.

Ahsante.
Mbele said…
Ndugu anonymous unayesema Nyerere aliwabagua waIslam na pia unaongelea mambo yake na kanisa, fanya subira. Kuna majungu mengi katika suala hili la Nyerere na wa-Islam.

Hayo majungu nayo napangia kuyaanika siku za usoni, kwa lengo la kutaka uthibitisho. Hapo tutakuwa tumemfanyia haki Mwalimu Nyerere, na tutakuwa tunawafanyia haki watoto wetu, ambao wanastahili elimu, si majungu.
Novat A.S.M said…
Ni kweli Mwalimu alikiri kuwa ujamaa umeshindwa pale alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mwaka 1995,kuwa ninanukuu 'kuuzungumzia ujamaa leo inahitaji kuwa na moyo wa kiuendawazimu hivi'mwisho wa kunukuu,hii alimaanisha kuwa ujamaa umeshindwa kiasi kwamba ukiuzungumzia leo watu hawawatakuelewa kabisa kiasi kwamba inahitaji moyo wa mwendawazimu kuendelea kuuzungumzia.Lakini mwalimu aliendelea kutuasa kuwa tunaweza kuuacha ujamaa lakini hatuwezi kuacha kijitegemea, alisisitiza kuwa kujitegemea kutaendelea kuwa valid siku zote na ni ole wetu kama taifa tukaacha filosofia ya kujitegemea,Huyo ndiye mwalimu aliyekuwa anaona mbali
Anonymous said…
Profesa Mbele na wasomaji wenzangu.

1. Kwanza Profesa nakupongeza kwa juhudi zako za kutaka kuuweka ukweli hadharani. Hakika hilo ni jambo jema. Aidha, ningependa wachangia hoja katika hili wapende kuweka maoni yatakayotuelimisha, na sio maneno ya mkato mkato.

2. Mimi siwezi kukubali au kukataa kama Mwalimu alisema ujamaa umeshindwa. Ingawa nimesikia hayo kwenye vyombo vya habari mfano 'Julius Nyerere, the elder statesman of post-colonial Africa, dies, aged 77' Indipendent Newspaper 15th October 1999. Maelezo hayo yako hata kwenye You Tube, ingawa sio kutoka kinywa cha Mwalimu; lakini imeripotiwa kuwa Mwalimu alikiri Kushindwa kwa mfumo wa Ujamaa na kujitegemea.

3. Wakati wa 'Operation Vijiji', itakumbukwa kuwa watu walihamishwa maeneo ya mijini kupelekwa kwenye 'vijiji vya ujamaa'. Mafanikio ya vijiji vya ujamaa kwa kweli na msingi ni kwamba hayakuwepo. Wengine waliuwawa na wanyama pori kwa kuhamishiwa katika 'vijiji' vilivyopangwa katika maeneo ya hatari.

4. MSINGI WA UJAMAA WA TANZANIA UNATOKANA NA AZIMIO LA ARUSHA. Mali za 'mabepari' zilitaifishwa na mihimili yote ya uchumi ikapewa serikali. Tukaingia kwenye ushirikiano wa Afrika Mashariki na kupata hasara kubwa 1977. Cha msingi ni kwamba katika hio mihimili ya uchumi,Serikali iliyoongozwa na Azimio la Arusha haikufanikiwa katika kuwaondolea watanzania maadui watatu (Umaskini, Ujinga na elimu)kama alivyolenga mwalimu.

5. ikumbukwe kwamba tumepewa misaada ya udugu katika ujamaa na jamhuri ya china ikiwemo TAZARA na Mradi wa Mpunga Rujewa, Mbarali ambao una kinu cha kuzalishia umeme na ni shamba la kipekee. misaada hiyo ilikuwa na ufanisi ilipokuwa inasimamiwa na wachina, Serikali ilipokabidhiwa; ilidorora! Ujamaa na Azimio la Arusha kinadharia ni muafakamzuri wa usawa na kutafuta maendeleo. Leo tunalalamikia mgao wa umeme, kama mdau aliyechangia anaesema anaitamani $100 anunulie mishumaa. Wakati wa kilele cha ujamaa na azimio la Arusha ilikuwa kuna mgao wa chakula --- DONA. Watu walikuwa wanaoga kwa harita na wanakunywa uji wa chumvi. Sasa kama hayo ndio mafanikio ya Ujamaa na Azimio la Arusha tuambizane.

6. Jambo la busara alilolifanya Julius Nyerere ni kung'atuka 1985, ingawa kwa kuwa alikuwa bado anapenda madaraka; akaendelea kuwa mwenyekiti wa CCM mpaka 1992. Aling'atuka kwa kuwa alishaamini kuwa hana tena mchango wa kuinasua nchi katika mgogoro wa uchumi aliokuwa ameshaiingiza kwa miaka 18 mfululizo tangu alipotangazia taifa azimio la arusha. Ali Hassan Mwinyi, licha ya kubughudhiwa katika utawala wake (Kwa sababu Mwenyekiti wa Chama aliendelea kuwa Mwalimu); alifanikiwa kuleta mageuzi ya Uchumi, kufungulia vyombo vya habari na vyama vingi. Watanzania leo wanapayuka watakavyo, hii imetokana na 'liberal' policies za Mzee Mwinyi. La msingi kabisa, ni baada ya Mwalimu tu kuachia uenyekiti na Azimio la Zanzibar likapitishwa.

7.Mwalimu alifanikiwa sana katika uongozi wake, lakini Sera ya Ujamaa na Azimio la Arusha vilishindwa. La kustaajabisha Sasa Tanzania sijui tujiite mabepari au? maana sielewielewi.

8. Profesa samahani kwa mchango mrefu, naamini hapa nitazua mjadala.
Simon Kitururu said…
This comment has been removed by the author.
Simon Kitururu said…
@NOVAT A.S.M:,,,
,....na ANONY wa July 2, 2011 10:13 PM,...

... NIMEEGEMEA KWELI kweli yenu,...

....labda kwa kuwa KWELI MPEKECHAYO labda yafanana sana na KWELI zangu kinamna katika hili SWALA.:-(
Anonymous said…
ukitaka khabari zote za NYERERE na UJAMAA, MUWAHI MZEE JUMBE KABLA HAJAFA PALE MJI MWEMA. ATAKUPA ISSUE ZOTE
Anonymous said…
kushindwa kitu,mzee mbele sio lazima ukili kwa maneno, au kutangaza. mbona hapa kwetu democrasia imetushinda, ni lini walitangaza?,mbona police wanalaumiwa kutokana na makosa wanayofanya na kila mtu anayaona makosa hayo (hata na wewe pia)ni lini walikiri wazi kuwa wanamakosa?
hivyo basi,kushindwa kwa ujamaa si lazima mpaka iwe kwa kauli ya mwalimu!
Chambi Chachage said…
Katika moja ya mahojiano yake ya mwisho kabla ya mauti kumchukua, Mwalimu alisema haya kuhusu hoja ya kushindwa kwa Ujamaa na Usoshalisti:

MJN: I still travel around with it [The Arusha Declaration]. I read it over and over to see what I would change. Maybe I would improve on the Kiswahili that was used but the Declaration is still valid: I would not change a thing. Tanzania had been independent for a short time before we began to see a growing gap between the haves and the have-nots in our country. A privileged group was emerging from the political leaders and bureaucrats who had been poor under colonial rule but were now beginning to use their positions in the Party and the Government to enrich themselves. This kind of development would alienate the leadership from the people. So we articulated a new national objective: we stressed that development is about all our people and not just a small and privileged minority.

The Arusha Declaration was what made Tanzania distinctly Tanzania. We stated what we stood for, we laid down a code of conduct for our leaders and we made an effort to achieve our goals. This was obvious to all, even if we made mistakes - and when one tries anything new and uncharted there are bound to be mistakes.

The Arusha Declaration and our democratic single-party system, together with our national language, Kiswahili, and a highly politicized and disciplined national army, transformed more than 126 different tribes into a cohesive and stable nation.

However, despite this achievement, they say we failed in Tanzania, that we floundered. But did we? We must say no. We can't deny everything we accomplished. There are some of my friends who we did not allow to get rich; now they are getting rich and they say `See, we are getting rich now, so you were wrong'. But what kind of answer is that?

The floundering of socialism has been global. This is what needs an explanation, not just the Tanzanian part of it. George Bernard Shaw, who was an atheist, said, `You cannot say Christianity has failed because it has never been tried.' It is the same with socialism: you cannot say it has failed because it has never been tried.

Chanzo: http://www.hartford-hwp.com/archives/30/049.html
Anonymous said…
sasa Mbele,hakuna majungu hapo ni ukweli mtupu.kushindwa ujamaa kwa nyerere ndiyo sababu iliyompelekea kung"atuka yeye mwenyewe bila kulazimishwa na mtu.Mwalimu anamzuri yake mengi na mengi mabaya :Alikuwa dictator hakukubali kushindwa ilihali tayali maji ya shingo.
Mbele said…
Anonymous, ufahamu wa ki-Ingereza umedidimia sana Tanzania. Hilo andiko aliloleta Ndugu Chambi ndio namna Mwalimu Nyerere alivyokuwa anajibu, miaka ya mwisho ya maisha yake, suali la kama ujamaa umeshindwa au la.

Anachosema Mwalimu ni kitu tofauti na hicho mnachowazia akina anonymous. Mimi kama mwalimu wa ki-Ingereza kiwango cha chuo kikuu hapa Marekani, napenda kukuthibitishia kuwa Mwalimu anaihoji hii dhana ya kwamba ujamaa umeshindwa. Mimi si anonymous, na kama ninachosema sio kweli, basi ni mimi ndiye nitakayepoteza heshima.

Kudidimia kwa ufahamu wa lugha ni janga la Taifa letu, ingawa wa-Tanzania wanalifanyia mchezo suala hili. Kupata fununu kuhusu maoni yangu, soma hapa.
Anonymous said…
on your last comment! Mbele..

Haambiliki! Lesson from the master..what are you trying to say exactly??

It is clear from the writing, he agreed on the falure of Ujamaa, but what he is trying to do, just like you Mbele, Diverting the Falure of Ujamaa in Tanzania by mentioning the falure of other Ujamaa of other countries on the whole wide world...ie Running from his responsibilities and his falure..he was a president of Tanzania, and not UN secretary general mandated for a charge of the countries of the world, he cowardly afraid to stand on his own feet...The Chinese realised their falure in 1980..(Go and do your homework Mbele)

As an english Teacher, I wont fancy you to be my teacher! Sorry !
Mbele said…
Anonymous wa 2:18 ambaye umeandika hapa kwa ki-Ingereza chako kibovu, ingekuwa vema kama ungejitambulisha, ili uwajibike kwa yale usemayo. Ningependa mjadala tuuweke kwenye kiwango cha taaluma ipasavyo, ambapo wahusika tunafahamika.

Anonymous wewe unatakiwa ujifunze kusoma kwa uangalifu kwani maelezo ya Mwalimu Nyerere, sio katika hii kipande kilichonukuliwa tu, bali katika mahojiano mazima, si ya mkato kama unavyodai.

Nyerere alijieleza tena na tena katika mahojiano miaka hii mwisho wa maisha yake, akifafanua na kusisitiza hilo alilosema hapa, ambalo ni kuhoji dhana ya kufeli ujamaa.

Wewe mwenyewe, kama umesoma dhana ya ujamaa alivyoileza katika maandishi na hotuba mbali mbali, dhana yenye vipengele vingi, kuanzia vya kifalsafa na kinadharia, hadi vya utekelezaji katika nyanja mbali mbali za maisha, huwezi kuja na hii dhana kuwa ujamaa ulifeli. Ndio maana Mwalimu Nyerere hatoi majibu ya mkato, kutokana na utajiri wa dhana nzima ya ujamaa kama nilivyogusia. Lakini watu wavivu wanataka majibu ya mkato.

Kwako anonymous, Nyerere ametoa jibu ambalo linaendana na ukweli kuwa ujamaa una vipengele vingi, na kwamba hata kama hiki au kile kilikwama, huwezi kusema ujamaa ulifeli.

Kwamba Nyerere haambiliki ni majungu. Je, ilikuwaje, miezi michache tu baada ya Uhuru, Mwalimu Nyerere alichapisha kijitabu kiitwacho "Tujisahihishe"? Ilikuwaje, miaka ya mwisho ya utawala wake, alianza kutetea dhana ya kuwepo vyama vya upinzani? Ilikuwaje hata kwenye haya mahojiano aliyoleta Chambi, Nyerere anakubali makosa? Majungu ya kwamba Nyerere haambiliki nilishayapangia muda wake wa kuyaanika. Tutaona watu wanavyojikanyaga.

Sihitaji kuwa na mwanafunzi kama wewe, wala sitafuti wanafunzi. Hao Wamarekani walioniomba mwaka 1990 nije niwafundishe wananitosha, na wanakuja wenyewe darasani kwangu.
Anonymous said…
,,
Anonymous said…
what Nyerere did on azimio la arusha declaring war against the middle class, the riches etc, instead of combating the incompetence, corruption within his own political elites...you simply cant do that, but what i inderstood is that he remained on the principals of ujamaa when the azimio was declared and practiced and subjected it to hard working people who worked hard for their own wealth..

And thats thuggish behaviours, and he then slowly transfering the whole econimics machines, ie industries, agricultural to the incompitent political elites only by how good their praise of the ujamaa, and that is stealing.

He then gathered the wealth brought about by the same people who he tried to slander to build the other industries and sectors of the economy and again give the control to the political elites, subsequately brought the country to his knees. He was like a spoilt kid with real atitude.

It was disaster, and thats the exact word used by many experts, but one thing for sure he was poetic, again copied from shakespear and translate to swahili. fact!

So tell me professor, may be im living in different plant, the success of a single goverment run industry,business or kijiji cha ujamaa, and thats was his vision for the whole country.. And if you ask me and 90% of the contributors of your blog on this thread or those of mjengwa, they are on position contrary to what you'r trying to say, it is simple ujamaa failed this nation. You are on your own professor..haambiliki just like your fellow techer Nyerere.

From the article posted above, He(Nyerere) simply saying ujamaa is a well written piece of paper which can't be implimented. Mao realised that and the subsequent leaders following Mao, have gone agreat length to their past mistakes and admissions to those falures.
In other words, in any society there must be a middle class, the rich and extreme riches, it is like any sport, you have those who are winning with pure talents and those who are comming second, third and so forth, and always the loosing team try harder next time, but you simly can't punish the winner, and try to put theory behind and saying we all can become a winner, it is unworkable, it only encourages laziness, no innovation, discourage motivation, and more importantly development..to adjust to the demand of those who cant compete, we have the system called taxes for the rich, that subsequently can be used to provide social services to the poor, thats where socialism fits in, similarly an approach taken by many european countries. But nyerere went opposite way, declaring war against those who worked hard, rather than learning from it.

Thats why im saying ujamaa is good piece if paper well written but unworkable.
Mbele said…
Mimi kama mmiliki wa blogu hii, ninashauri turudi kwenye ajenda. Ajenda ilikuwa kubainisha maneno ya Mwalimu Nyerere. Ilikuwa ni kuondoa majungu yanayonadiwa kuwa ni maneno ya Mwalimu Nyerere. Ilikuwa ni kuhifadhi kwa usahihi maneno ya Mwalimu Nyerere.

Masuala mengine tunaweza kulumbana, masuala kama je, Nyerere alikuwa dikteta? Au je, ujamaa unafaa, au ulishindwa? Na kadhalika. Sote tuna uhuru wa kuyajadili hayo. Ni haki yetu.

Lakini ajenda ya kuhakikisha kuwa maneno tunayosema ni ya Mwalimu Nyerere yawe kweli ni yake, ni ajenda isiyo na ubishi. Watafiti na wanataaluma wote wanataka hivyo. Pia ni suala la haki mtu kunukuliwa maneno yake kwa usahihi kabisa. Kumsingizia mtu kasema kitu ambacho hakusema ni kumkosea haki.

Kwa hivi, napenda wanaotaka kuendelea na mjadala huu, warudi kwenye ajenda.

Napenda kurudi kwenye ile nukuu aliyoleta Chambi, ambayo ni kweli maneno ya Mwalimu. Nilimwambia anonymous kwamba katika maneno yale, Mwalimu hakusema kuwa ujamaa umeshindwa.

Anonymous wa July 4, 2:18pm, sijui kama ni yule yule wa mwanzo, au mwingine, akaja na kauli kuwa katika maneno yale, Mwalimu Nyerere amekiri kuwa ujamaa umeshindwa. Anonymous huyu karudia hilo neno lake "falure" mara kadhaa, na nadhani alitaka kuandika "failure." Akaibeza kauli yangu kuwa mimi ni mwalimu wa ki-Ingereza ambaye najua ninachosema.

Sasa basi, kwa nini nimesema kuwa katika ile nukuu, Mwalimu hakusema ujamaa umeshindwa?

Nadhani kilichompotosha anonymous huyu ni pale Mwalimu aliposema: "The floundering of socialism has been global."

Ieleweke kuwa kabla ya kusema hivyo, Nyerere alishaanza kwa kusema kuwa kauli kuwa ujamaa umefeli ni lazima tuikatae. Pili ndipo tuje kwenye hii sentensi ambamo anakiri kuhusu "floundering" ya ujamaa sehemu mbali mbali za dunia.

Anyonymous, kwa kutojua ki-Ingereza, amedai kuwa Nyerere kakiri "falure" ya ujamaa. Aonymous huyu amedai kuwa Mwalimu kakiri "falure" ya ujamaa sehemu mbali mbali za dunia.

Ukweli ni kuwa neno "flounder" halimaanishi kushindwa. "Flounder" ni kwenda mbele kwa matatizo matatizo, ukiwa unachechemea, unayumba, unajikwaa, unapepesuka kama anavyofanya mlevi, lakini unasogea mbele.

Hii ndio maana ya "flounder," ambayo huyu anonymous anayejitamba anajua ki-Ingereza ameshindwa kuielewa.

Ujumbe wangu kwa huyu anonymous wa July 4, 2:18 ni kuwa kwenye hii nukuu, Mwalimu hajasema kuwa ujamaa umeshindwa. Kumpinga kwa msimamo wake ni jambo tofauti, na ni ruksa. Lakini tumtendee haki kwa kuyahifadhi, kuyanukuu, na kuyatafsiri maneno yake kwa usahihi.
tz biashara said…
Profesa pole na kazi...Mimi ni mmoja ya wale waliokuwa wakipanga foleni ya kununua bidhaa kama chakula na sabuni za miche.Mimi ninachokiona hapo ni muda wa mtu kuongoza nchi na kwa staili gani.Nyerere alikuwa kiongozi ambae anasikilizwa na wengi na labda tuseme kipaji alichokua nacho ni kikubwa.Lakini alichokikosea ni siasa aliokuja nayo ndio iliyofanya wengi kumkataa kwa sababu hali iliyokuwepo wakati huo na kwakua ni "full independent".Kama ingekuwa au atatokea kiongozi kama nyerere kuongoza hii nchi lakini sio kwa siasa ya ujamaa basi labda corruption itapungua na viongozi na wafanyakazi wa serikalini watawajibika ipasavyo.
Anonymous said…
tetea Mfumo kristo Mzee Mbele mimi Muro
Anonymous said…
prof wangu usiseme hutaki umfundishe mtukamahuyo unakosea maana mimi kunaelimu kubwa unanipa hapo kwenye blog yako pamoja ni anony halafu usiwe na hasira wengine tunafanya hivyo tupate busara zako.halfu huyo alyejitaja muro kutetea mfumo kristo kaishiwa na huyo kama ni mmoja wao hao amshukuru mwalimu nyerere bila hivyo sijui kama wangeipata hiyo elimu
Mbele said…
Anonymous wa Julai 8, 9:57 am, shukrani kwa nasaha zako. Kuhusu Muro, nahisi ni Muro ambaye huwa nalumbana naye Facebook. Nikizingatia kuwa nahisi ni yeye, napenda kukuhakikishia kuwa ujumbe wake nimeupenda.

Tuna kajadi ka kuchokozana kule Facebook, na kwa upande wangu naona tumekuwa kama watani wa jadi :-)
emu-three said…
Kuna vitu viwili hapa naomba tujue, au nielimishwe, kuwa `kushindwa ' huko ni kutokana na matamshi yake mwenyewe kuwa alitamka kuwa ujamaa umeshindwa, au kwa siasa yenyewe, au niseme kwa uongozi wake mwenyewe Nyerere ambao ulisimamia kwenye Ujamaa na kujitegemea na azimia la Arusha? Nauliza tu waungwana

Popular posts from this blog

Kumbukumbu ya Kuzaliwa

Tenzi Tatu za Kale

Pesa za Majini