Tuesday, May 22, 2012

Makaa Yetu ya Mawe Yanakwenda Wapi?

Hapa ni Bandari ya Ndumbi iliyopo mwambao mwa ziwa Nyasa.Bandari hii inatumika kusafirishia makaa ya mawe ambayo yanachimbwa katika kijiji cha Ngaka wilayani Mbinga mkoani Ruvuma.Takwimu zinaonesha kuwa kila wiki zaidi ya tani 600 za makaa ya makaa ya mawe zinasafirishwa kupitia bandari hii kupelekwa sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi.Hata hivyo hakuna anayefahamu ukweli kuhusu kile ambacho kinasafirishwa kupitia bandari hiyo ambayo haina ofisi muhimu za serikali.
 (Picha na maelezo na Albano Midelo, Maendeleo ni Vita)

4 comments:

tz biashara said...

Yanakwenda kwa wenye kujua kuyatumia.Tatizo nchi ina viongozi wasio na uchu na nchi.Kiongozi alie na uchu wa nchi yake basi atajituma kisawasawa na bila ya kumuonea haya mtu.Kama unamjua kiongozi hajawahi kuonyesha matumaini ktk kazi yake yanini unampa kazi.Na kama unaona madudu ni mengi kwanini humfukuzi kazi.

Profesa...utajiri uliokuwapo nchi hii ilipaswa kutumika kwa manufaa ya wananchi.Wananchi walipaswa kupewa elimu ya bure tena mpaka university.Lakini walijuwa kama watawapa elimu wananchi wasingeweza kuiba na kuwanufaisha wa nje.Kwa hiyo thamani ya mwananchi huwezi kuiweka sawa na wa nje.Miaka 50 ya uhuru ulikuwa ni feki kwasababu hakionekani kilicho huru.

Miaka 50 kwa mimali iliyokuwepo basi vijiji vyote vingefaidika kwa maji,umeme,shule nzuri mpaka sekondari,hospitali n.k.Lakini leo inabidi vijana wakimbie vijijini waende wakafanye kazi za umachinga.

Je kama nchi imewashinda kwanini hawakubali????Kwanini wanauza ardhi ya Mtanganyika??Wanavijiji wengi hivi sasa kunaulalamishi ya ardhi yao kuuziwa wawekezaji wazungu mfano upo hapo Mororgoro.

Tusubiri katiba kama kweli itakuwa ya kumtetea mwananchi na nchi yake.

GOD BLESS TANZANIA

Simon Kitururu said...

Mmmmmmmh!:-(

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Yanakwenda kule kule zinakokwenda almasi za Mwadui....

Nilikwenda pale nikayaona maalmasi laivu kidogo nilie. Ndani ya mgodi kuna watu wanaendesha Rolls Royce lakini ukitoka nje tu Wasukuma wako nyang'anyang'a hata kandambili hawana.

Mbele said...

Nimekumbuka kuwa niliandika makala inayosema kuwa sera ya madini Tanzania ni wizi mtupu. Isome, hapa

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...