Friday, May 11, 2012

Mrembo

Katika kitabu changu kiitwacho Africans and Americans: Embracing Cultural Differences, pamoja na masuala mengine, nimeongelea suala la urembo. Nimesema kuwa dhana ya urembo ni tofauti katika tamaduni mbali mbali na katika mazingira mbali mbali. Kwa mfano, nimenukuu hadithi ya mapokezi ya kabila la Efik-Ibibio, Nigeria, inayoelezea unene kama kigezo cha urembo: There was once a very fat woman who was made of oil. She was very beautiful and many young men applied to her parents for permission to marry her and offered a dowry; but the mother always refused.

Kifungu hiki nimekinukuu katika ukurasa 54 wa kitabu changu, na naweza kutoa tafsiri hii: Alikuwepo mwanamke mnene sana aliyeumbwa kwa mafuta. Alikuwa mzuri sana na vijana wengi waliwaomba wazazi wake ruhusa ya kumwoa wakatoa mahari, lakini mama mtu daima alikataa.

Katika kitabu changu cha CHANGAMOTO: Insha za Jamii, kuna sehemu ambayo inaongelea mashindano ya urembo, kukumbushia kuwa kila jamii inayojitambua na kujiheshimu ina dhana yake na vigezo vyake vya urembo. Mambo hubadilika, ila jambo la kulitafakari ni mchakato wa mabadiliko hayo ni wa aina gani na misingi yake ni ipi. (Picha niliyoweka hapa nimeiona Facebook}

3 comments:

Anonymous said...

nikweli Professa Mbele unene ni ulembo hasa kwetu huku afrika unasisimua hata mwanamke mnene akipita Kariakoo ndiye anaye kimbiliwa na vijana kuliko wale wembamba kwahiyo hizo ndio tamaduni zetu za kiafrika

tz biashara said...

Mimi naona ya kwamba unene ni maumbile ya mtu na urembo unatokana na jinsi unavojiweka hasa ktk mavazi ambayo yataendana na mwili wako.

Unaweza kuwa mnene na ukavaa nguo fupi na kuonyesha idadi kubwa ya mwili wako na iliyokubana na hatimae ukawafanya wengi wakukodolee macho na sio kwa uzuri wako ila kwa kuchukiza kwako kwa kuonyesha minyama uzembe.

Lakini mnene huyohuyo akavaa nguo nzuri maridadi ambayo haitomuonyesha minyama uzembe,basi pengine wapo watamkodolea macho kwa kumtamani lakini na kumuekea heshima kitu ambacho muhimu kupendwa na kupewa heshima.

Umbile la unene,wastani au wembamba ni chaguo la mtu vile mapenzi yake yanapofika.

Sasa huu urembo wa kutengena kupitia madawa kwakweli ni ugonjwa tu mimi nionavyo,kwasababu hujui madhara yake baadae.Uzuri ni ule ulioumbwa na mwenyezi mungu peke yake na ni dhambi kujibadilisha maumbile yetu ikiwa tumeshatunukiwa na mwenyezi mungu.

emuthree said...

Urembo wa mtu ni kile kinachomvutia machoni mtu,au hisiani,....mrembo au urembo wa yule, sio lazima uwe sawa na mimi.
Kutokana na kutojiamini, watu wanaamua kujikarabati,...kumbe hawajui kuwa ule uasili wake,kulikuwa na watu wanaupenda,...na alivyojikarabati, wale waliokuwa wakimpenda kwa asili yake ameshawapoteza, na kupata wengine ....na tukumbuke ukachakachuaji wa mwili ni wa muda, hauna thamani....
Ni hayo ya kwangu tu

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...