Tamasha la Kimataifa Mjini Faribault

Leo nilikuwa mjini Faribault kushiriki tamasha la kimataifa International Faribault Festival. Nimeshiriki tamasha hilo kwa miaka kadhaa kama mwalimu, mwandishi, na mtoa ushauri kuhusu masuala ya tofauti za tamaduni.

Hapa kushoto ni wanafunzi waliokuwa wanaongoza shughuli katika ukumbi mkuu wa tamasha. Shughuli hizo zilikuwa ni maonesho ya burudani, hasa ngoma za mataifa mbali mbali.


Watu wa kila rika walihudhuria, kama ilivyo kawaida katika matamasha haya hapa Marekani. Kulikuwa ni michezo mbali mbali ya watoto.


Nilikwenda na vitabu vyangu na machapisho mengine, kama inavyoonekana picha ya mwisho hapa kushoto. Kama kawaida, vitu hivyo huwa ni kivutio kwa watu na wanafika hapa mezani kuangalia na pia kuongea nami. Hiyo leo ilikuwa ni hivyo hivyo. Niliongea na watu wengi, kuanzi watoto hadi wazee.

Kwa mfano, huyu bibi anayeonekana kulia, mwenye nywele nyeupe, tuliongea sana. Alinieleza kuwa anamfadhili binti yatima aliyeko Ethiopia. Tuligusia tofauti za tamaduni, nikamweleza jinsi ilivyo muhimu kuzitafakari, kwani zinaathiri tabia, mawasiliano, na mengine. Mama mwingine aliyekuja hapa mezani pangu alisema anafundisha ki-Ingereza kwa wahamiaji kutoka nchi mbali mbali. Hapa Marekani, program hii inajulikana kama ESL, ambayo kirefu chake ni English as a Second Language. Basi, tuliongelea kidogo jinsi tofauti za tamaduni zinavyojitokeza katika programu hiyo, akanunua kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences.

Comments

Popular posts from this blog

Kumbukumbu ya Kuzaliwa

Tenzi Tatu za Kale

Pesa za Majini