Monday, May 16, 2022

VITABU VYANGU, NAFSI YANGU

Vitabu vyangu si vitu vilivyo nje yangu. Ni sehemu ya nafsi yangu, kama kilivyo kichwa changu au ulivyo moyo wangu. Haiwezekani kuvitenganisha na mimi mwenyewe.

Ninaandika vitabu si tu ili watu waifahamu mada, bali pia ili wanifahamu. Kwa hiyo, sielei angani kwa nadharia na hoja zisizofikika kirahisi. Ninaongelea mambo yanayomgusa binadamu. Vitabu hivi ni sauti yangu na pumzi yangu.

Nitakapokuwa siko diniani, vitabu hivi vitaendelea kuongea na walimwengu, vikiwasilisha sauti yangu. Kwa njia ya kazi zao, waandishi tangu kale wametamani na wamefanikiwa kuishi hata baada ya kufariki.

Gilgamesh, shujaa wa kale wa Mesopotamia, alitamani hivyo, akataka kuandika jina lake, lisitoweke. Akina Shakespeare na Shaaban Robert bado tunao, kadhalika akina Tolstoy, Muyaka, Achebe na wengine kwa maelfu.

2 comments:

Father Kidevu said...

Hongera sana kwa kazi nzuri. Kazi yako inanivutia sana

Mbele said...

Asante sana, Father Kidevu, kwa ujumbe wako. Nafurahi kusikia kuwa unavutiwa na kazi yangu. Namshukuru Mungu, mwezeshaji wa yote, nawe nakutakia kila la heri.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...