Sunday, May 22, 2022

Huenda Nikaandika Kitabu Kingine Kuhusu Tamaduni

Tarehe 25 Agosti, 2021, nilichapisha kitabu, Chickens in the Bus: More Thoughts on Cultural Differe=-ians and Americans: Embracing Cultural Differences." Baada ya kuchapisha vitabu hivi, niliona sina haja ya kuandika kitabu kingine juu ya tamaduni.

Lakini, wiki kadhaa zilizopita, nilizindua programu ya mtandaoni, "Cross Cultural Conversations," ambayo naendesha kila Jumamosi. Ninaongea kupitia Zoom na kuwashirikisha wasikilizaji katika maongezi juu ya mada mbali mbali kuhusu tofauti baina utamaduni wa Afrika na wa Marekani.
Katika kufanya hivyo, nimejikuta nikizama zaidi katika masuala niliyoongelea katika vitabu vyangu, na ninaibua pia mengine au mitazamo ambayo haikuwemo vitabuni. Nikiendelea namna hii, nitachapisha kitabu kingine, labda kiitwe "Cross Cultural Conversations." Itachukua muda, bila shaka miaka kadhaa.

4 comments:

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Nangoja kwa hamu sana kupata nakala yangu kaka

Mbele said...

Ndugu Mhango

Asante kwa ujumbe wako. Ni miaka imepita tangu tuwasiliane mara ya mwisho, lakini muda wote huu nimekuwa na nia ya kuandika ujumbe rasmi kuhusu zawadi ya vitabu vyako ambavyo ulinipa miaka iliyopita. Ujumbe uliohitajika na unahitajika ni wa shukrani na mambo ya aina hiyo. Sijasahau, na nasubiri siku muafaka.

Kuhusu hiki kitabu ninachowaZia, panapo majaliwa nitaandika tu.

Best African Safari Tours said...

Beautiful post. Thank you for sharing.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Kaka wala usijali. Siku ukipata fursa muafaka haina neno. Hata hivyo, kwa hayo machache uliyokumbushia umeshukuru. Nami nashukuru kwa kunitumia kitabu chako mahiri juu ya mila na maingiliano yake. Habari njema, kama watamaliza balaa la ukame na ukosefu wa umeme, nimealikwa J'berg Afrika Kusini kuzindua kitabu changu kinachotegemea kutoka hivi karibuni ambacho nilimshirikisha mwenzangu Profesa toka Uganda anayefundisha hapa Kanada.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...