Friday, August 13, 2010

Niko Morogoro: Mji Kasoro Bahari

Nimekuwa Morogoro tangu juzi, nikipunga upepo na kutembelea sehemu kadhaa.

Morogoro ni mji maarufu katika Tanzania. Uko katika njia kuu za usafiri baina ya Tanzania na nchi za Afrika ya kati na kusini.
Ni mji uliosifiwa sana na mwanamuziki maarufu Mbaraka Mwinshehe, kwa uzuri wake, na uzuri wa mandhari yake. Katika sifa hizi, aliongelea jinsi maji yanavyotiririka milimani Morogoro. Wenyeji wa hapo, wa-Luguru, ni maarufu miongoni mwa sisi watani zao, kwa jinsi nao wanavyojivunia huu mji, wanaouita Mji Kasoro Bahari.

Kila ninapopita Morogoro, nakumbuka umaarufu wake. Hapo kuna shule na vyuo maarufu tangu zamani, kama vile Kilakala, Kigurunyembe, Mzumbe, na Sokoine. Miaka ya karibuni kimeanzishwa pia chuo kikuu cha Ki-Islam. Ni mji muhimu kwa upande huu, wa elimu.

3 comments:

Bennet said...

Nilikuwa hapo kama wiki mbili zilizopita, nilitembelea ofisi za wakala wa mbegu wa taifa, chuo cha kilimo Sokoine pamoja na mashamba ya mbegu ya Samaki morogoro mjini na Kingolwira, pia nilifika hadi mzumbe.
Mji ni mzuri, msafi na hakuna foleni za magari kama dsm

Mbele said...

Ninapangia kuandika makala zingine kuhusu Morogoro na sehemu nyingine nilizotembelea. Nimerudi hapa Marekani jana, na picha nyingi sana za maeneo mbali mbali ya Tanzania.

DEUS THOMAS LIGANGA said...

kazi nzuri hongera

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...