Mh. Balozi Peter Kallaghe Afutarisha UK

Haya ndio mambo yanayotakiwa Tanzania. Nimevutiwa na kila kitu katika video hii, kuanzia ule wimbo mtamu wa kuienzi nchi yetu na utambulisho wetu kama wa-Tanzania, hadi mshikamano baina ya wa-Tanzania, na nasaha murua zilizotolewa na wasemaji. Mungu Ibariki Tanzania.

Comments

tz biashara said…
Prof..hii imenifurahisha sana nilikuwa sijawahi kuiona lakini inapendeza kuona amani bado ipo ktk nchi yetu ni baadhi ya wajinga fulani ndio wenye kuleta udini usio na kichwa wala mguu.Unajua kunasiku nimesoma malalamiko ya mtu alipeleka ktk blog ya mjengwa na michuzi.Alilalamika kuhusu balozi wetu ambae yupo Saudi Arabia hataki kuonana na watanzania.Kwahiyo sisi tunabahati huku UK kwa balozi wetu.
Mungu Ibariki Tanzania.
Mbele said…
Shukrani kwa ujumbe. Hiyo ya Saudi Arabia nayo niliiona kwa Michuzi. Hiyo ya Uingereza imenivutia kwa sababu hizo hizo ulizogusia.

Popular posts from this blog

Tenzi Tatu za Kale

Kumbukumbu ya Kuzaliwa

Filamu ya "Papa's Shadow:" Fursa ya Kuitangaza Tanzania