Tuesday, March 27, 2012

Kunywa Maji Badala ya Ulabu

Kwa siku kadhaa sasa, nikiwa katika kutumia dawa nilizoandikiwa na daktari, ni marufuku kukata ulabu. Badala yake, kinywaji changu ni maji tu. Nikikaa mahali, hata baa, kinywaji changu ni maji tu.








Mwanzoni, nilidhani itakuwa adhabu kali kuziangalia chupa za bia baridi katika joto hili la Dar es Salaam bila kunywa hata glasi moja. Lakini nimegundua kuwa kunywa maji kuna raha yake. Ningejiona shujaa iwapo ningeweza kuendelea hivyo hivyo maisha yote.

3 comments:

Rachel Siwa said...

Nami nakuombea usirudie tena kwenye urabu,Raha ya Maji na iendelee daima,Pole lakini ninamatumaini dawa zitafanya kazi vyema.Tupo pamoja kaka.

Yasinta Ngonyani said...

Hakuna kichowezekana Prof. nakushauri endelea hivyo UTAWEZA TU..KAMA UNAWEZA SASA HAKIKA UTAWEZA.. Nafurahi kuona au kusikia unaendelea vema ..pamoja daima!!!

Mbele said...

Nashukuru kuwa tofauti na zamani, siku hizi sina hamu ya bia kama miaka ya zamani. Nakaa miezi mingi bila hata kuonja glasi moja.

Pamoja na kuwa tunaelimishwa na wataalam wa afya madhara ya bia, mimi mwenyewe najisikia kufaidika na hii hatua ya kupunguza kabisa au hata kuacha ulabu. Kila siku naona akili yangu iko timamu, tayari kufanya mambo muhimu ya kusoma, kufundisha, na kuandika.

Nasikia kichwa changu kiko katika hali hiyo nzuri muda wote, tofauti na zamani, ambapo siku zingine mtu ulishindwa hata kuamka kitandani kwa kuumwa na kichwa sana kama vile kinapasuka, sababu ya ulabu wa jana yake.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...