Monday, August 15, 2016

Msomaji Wangu Mpya

Msomaji mwingine wa kitabu changu Africans and Americans: Embracing Cultural Differences amejitokeza mtandaoni. Tarehe 29 Julai, katika ukurasa wake wa facebook, msomaji huyu, Seena, amekisifu kitabu hiki kama ni "Beautifully well written book."

Seena ni msomi mzaliwa wa Ethiopia. Ni mwanaharakati wa masuala za haki za binadamu na hasa wanawake na watoto. Pia ni mwandishi, ambaye kitabu chake, The In Between: The Story of African-Oromo Women and the American Experience, nilikiongelea katika blogu yangu ya ki-Ingereza. Katika picha hapa kushoto, ninaoneka naye, nikiwa nimeshika kitabu chake, siku alipokiongelea mjini Minneapolis.

Tangu nilipomfahamu Seena, nimevutiwa na ari yake ya kupigania haki. Ana taasisi yake ambayo aliianzisha kwa ajili ya kuhamasisha elimu ya wasichana katika eneo la Oromia, nchini Ethiopia, na aliniomba niwe mshauri mojawapo katika taasisi hiyo. Ninafurahi kushirikiana naye. Ninahisi kuwa Mungu akimjalia maisha marefu, atakuja kuwa kiongozi maarufu Afrika na ulimwenguni.

4 comments:

Khalfan Abdallah Salim said...

Prof, je kitabu chako kinapatikana hapa Nairobi, Kenya? Pili, nikumbushe bookshop yeney kitabu chako Dar es Salaam. Wiki ijayo huenda nikawa nyumbani, ninunue.

Ahsante.

Mbele said...

Ndugu Khalfan Abdallah Salim

Shukrani kwa ujumbe. Kitabu changu hiki hakipatikani katika maduka huko Kenya. Samahani, lawama ni yangu. Jaribu kuulizia Arusha, Tanzania, simu namba 255 784 297 504, imborutours@gmail.com.

Kinapatikana mtandaoni, kama vile Amazon.com na lulu.com

Unknown said...

Professor ninaweza kupata e-mail address yako kwa mawasiliano zaidi juu ya kuomba udhamini kusoma masomo ya umahiri United States. Ni ombi tu, ninahitaji msaada wako.
Joshua Lutambi

Mbele said...

Ndugu Kisare Joshua, Unaweza kuniandikia kwa kutumia anwani hii: josephmbele@yahoo.com

Kila la heri.

J.L. Mbele

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...