Tarehe 8 Agosti, nilikwenda Rochester, Minnesota, kuhudhuria mkutano wa bodi ya Rochester International Association (RIA). Tunakutana mara moja kwa mwezi. Katika ajenda ya tarehe 8, yalikuwepo mambo yanayonihusu moja kwa moja, ambayo ninapenda kuyaelezea hapa.
Moja ni kuwa wanabodi tuliohudhuria tuliulizwa na rais wa bodi, Brian Faloon, iwapo tutapenda kuendelea kuwa wajumbe mwaka ujao. Wote tulikubali. Mimi kama mwanabodi mpya kuliko wote, nilivutiwa na jinsi wajumbe walivyo na moyo wa kujitolea. Nilikubali kwa sababu ninathamini mchango wa RIA katika jamii. Kwa upande wangu, kutumikia RIA kumeniwezesha kufahamika katika mji wa Rochester. Kwa mfano, kupitia RIA niliweza kutoa mhadhara chuo kikuu cha Minnesota Rochester.
Pili ni kuwa RIA imesisitiza kuafiki pendekezo nililotoa siku zilizopita la kuonyesha filamu ya Papa's Shadow mjini Rochester. Bodi ilipendekeza kwamba onesho lifanyike kupitia maktaba ya Rochester. Tutafuatilia, ili filamu ionyeshwe hivi karibuni.
Jambo jingine ni kuwa mwanabodi Kristin Faloon aliwaeleza wanabodi kuhusu mhadhara niliotoa katika kikuu cha Winona, ambao yeye na mumewe Brian walihudhuria. Sikutegemea Kristin angeongelea tukio lile, lakini ilionekana wazi kuwa walifurahishwa na mhadhara ule, akasema kuwa walijifunza mengi. Kwa kuzingatia hadhi ya Brian na Kristin katika jamii, maoni yao yana uzito mkubwa. Nimewaandikia ujumbe kwamba sitawaangusha katika mihadhara ya baadaye.
Zaidi ya hayo, mkutano wa RIA umenifungua macho kuhusu taasisi zinazofanya shughuli zinazofanana na zangu katika kuendeleza maelewano baina ya watu wa tamaduni mbali mbali. Mbali ya Diversity Council-Rochester, ambayo niliifahamu, niligundua pia kuwa kuna kitengo katika Mayo Clinic kinachoshughulika na masuala ya kujenda na kustawisha mahusiano baina ya watu wa tamaduni mbali mbali. Ninatarajia kuwa tutakuwa na fursa ya kushirikiana kwa namna moja au nyingine.
Showing posts with label kujitolea. Show all posts
Showing posts with label kujitolea. Show all posts
Friday, August 11, 2017
Monday, August 7, 2017
Global Minnesota Wameniletea Kifuta Jasho
Juzi, tarehe 5, niliandika katika blogu hii kwamba nilikuwa nimepata barua ya shukrani kutoka Global Minnesota, kufuatia mhadhara niliotoa. Leo, bila kutegemea, nimepata cheki kutoka kwao, kama kifuta jasho.
Sikutegemea, kwani tangu mwanzo waliponialika kutoa mhadhara na hata baada ya mhadhara, sikuwa na hata fununu kwamba kuna kifuta jasho. Nami sikufikiria wala kutegemea. Nilichojali ni kufanya kazi waliyoniomba kufanya, yaani kujadili mada ya "African Folktales to Contemporary Authors."
Ninaongozwa na nasaha ya wahenga kwamba tenda wema nenda zako; usingoje shukrani. Kama nilivyosema katika blogu hii, mengine ni matokeo. Sijawahi kukataa mwaliko wa kwenda kutoa mhadhara kwa sababu ya malipo.
Watu wanaonihimiza nisitoe huduma bila malipo ninawaambia kuwa kuna baraka katika kuwasaidia watu. Fursa ya kutoa mhadhara ni ya manufaa kwangu, kwani inaniongezea uzoefu na kuniwezesha kujitathmini ufahamu wangu, hasa katika kipindi cha masuali na majibu. Vile vile matangazo ya mhadhara yanayoandaliwa na kusambazwa na wale wanaonialika yananiongezea kufahamika.
Mara nyingi, huwezi kujua watu unaowahutubia ni akina nani katika jamii. Nimeshuhudia baada ya mhadhara watu wakijitokeza na kujitambulisha kwangu na kuniuliza iwapo nitakuwa tayari kuhutubia kwenye taasisi au jumuia zao. Mwaliko moja unazaa mialiko mingine. Ninasema hayo ili kuwashawishi wale wanaosita kutoa huduma bila kuahidiwa malipo. Hakuna hasara, bali ni faida.

Tuesday, February 3, 2015
Wa-Marekani na wa-Tanzania: Tofauti za Tamaduni
Leo, katika ukurasa wake wa "Facebook," Ndugu Maggid Mjengwa aliandika: "Leo Nimepokea Wafanyakazi Wa Kujitolea Kutoka Marekani..."Wa-Marekani hao, ambao anaonekana nao katika picha hapa kushoto, wamefika Iringa kujitolea katika Kwanza Jamii, kampuni inayoendesha gazeti na redio. Maggid hakutuambia watakaa muda gani hapo Iringa, lakini nilijibu ujumbe wake "Facebook" namna hii:
"Safi sana. Ninapoona au kusikia mambo ya aina hii, wazo linalonijia akilini ni kuwa muhimu wageni wapate mtu wa kuwaelezea angalau yale ya msingi kuhusu tofauti kati ya utamaduni wa-Marekani na ule wa wa-Bongo, na wa-Bongo pia waelezwe kuhusu tofauti kati ya utamaduni wao na ule wa wa-Marekani. Hii ni kwa ajili ya kurahisisha shughuli na maisha kwa pande zote mbili. Kila la heri."
Suala hili nililoongelea ni muhimu hasa katika dunia ya utandawazi wa leo. Hao wageni wanapokuja kwetu na sisi tunapoenda kwenye nchi zao, ni mihumu kulizingatia, ili kufanikisha shughuli na mahusiano baina yetu. Nimeandika kuhusu tofauti baina ya utamaduni wa wa-Marekani na wa-Afrika katika kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences, ambacho nashukuru kwa jinsi kinavyowasaidia watu wanaokisoma, kama ilivyoelezwa hapa na hapa.
Hilo ni suala ninalolishughulikia sana katika utafiti, mihadhara na warsha. Hiyo picha hapa juu tayari inanipa vidokezo muhimu. Ninaona jinsi hao wasichana walivyomwangalia Maggid usoni, na yeye ameangalia chini. Hapo Mjengwa anaonyesha heshima kwao, kwa mujibu wa utamaduni wetu wa ki-Tanzania na ki-Afrika kwa ujumla.
Nao hao wasichana, kwa mujibu wa utamaduni wa Marekani, wanaonysha heshima kwa kumwangalia Maggid usoni. Huenda wanashangaa kwa nini hawaangalii usoni. Hilo suala la kuangaliana usoni ni moja ya yale ninayoyaongelea katika kitabu changu:
Kama hii picha ingekuwa ni video, ingenipa fursa ya kusema mengi zaidi.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Ukizunguka mitaani Dar es Salaam, utakuta matangazo mengi ya waganga wa kienyeji. Waganga hao wanatoka sehemu mbali mbali, kama vile Sumbaw...
-
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...