Thursday, May 6, 2010

Vitabu Pepe

Kadiri siku zinavyopita na mabadiliko ya aina aina kutokea, yakiwemo mabadiliko ya tekinolojia, lugha nayo inawajibika kukabiliana na mabadiliko haya.

Katika kuyamudu mabadiliko katika uwanja wa uandishi wa barua, kwa mfano, leo hii tuna kitu kiitwacho barua pepe. Zamani tulizoea barua ya karatasi na bahasha. Lakini leo tunaandika barua pepe, bila karatasi.

Kama ninavyoeleza hapa na katika kitabu cha Changamoto, ulimwengu wa vitabu nao unabadilika kufuatana na mabadiliko ya tekinolojia. Leo vitabu vinaandikwa na kusomwa bila karatasi, sawa na barua pepe. Sasa sijui vitabu hivi tutaviita vitabu pepe au vipi.

3 comments:

Fadhy Mtanga said...

Kaka Mbele nami ni mmoja wa wanaoishukuru sana teknolojia na maendeleo yake. Nami mara kadhaa hujishushia vitabu pepe kutoka mtandaoni. Nami niliwahi kuweka kitabu pepe cha mashairi niliyoyaandika hapa www.poemhunter.com/fadhy-mtanga

Mbele said...

Ndugu Mtanga, kwanza, kile kitabu nilichokuahidi nimeshakiweka katika sanduku nitakalosafiri nalo kuja Tanzania, ili nisije nikakisahau.

Nimefurahi kuona tungo hizi zako hapa.

Sasa, hatua ambayo ningependekeza ni kuwa siku zijazo uchapishe kitabu au vitabu kama ninavyofanya mimi kule lulu.

Kitabu chako unakichapisha mtandaoni kama ulivyochapisha mashairi yako. Lakini mtu anaweza kushusha mashairi yako akayasoma kwenye karatasi.

Hii ni sawa na vitabu vyangu. Nimevichapisha mtandaoni, lakini watu wanaviagiza na vinatengenezwa hapo mtandaoni kama vitabu halisi na wao wanapelekewa sawa na vitabu vingine tunavyovijua.

Lakini vitabu vyangu hivyo vinapatikana pia kama vitabu pepe kweli, kwa maana ya kwamba vinaweza kusomwa tu kwa kutumia kifaa maalum cha kushushia na kusomea bila karatasi.

Kila kitabu ninachokichapisha hapa lulu.com kinapatikana kwa namna hizo mbili, yaani kama kitabu halisi na pia kama kitabu pepe.

Fadhy Mtanga said...

Prof Mbele, awali ya yote napenda kukushuru kwa kuniwekea hicho kitabu. Natanguliza shukrani zangu za dhati.

Pia nashukuru kwa maelekezo yako juu ya kuchapa vitabu kupitia lulu.

Nitafanya hivyo hivi sasa kwani tayari nina mkusanyiko wa mashairi mengi.

Pale nitakapokwama nitaomba maelekezo yako.

Nakutakia kila la kheri. Nakusubiri kwa hamu Tanzania.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...