Friday, June 10, 2011

Marufuku Kusaidia Watoto wa Mitaani

Chanzo: Blogu ya Mwenyekiti Mjengwa

8 comments:

Simon Kitururu said...

Kazi ipo!

Anonymous said...

This is too much. Wanataka kula na hata za watoto wa mitaani. Wameona hiki kidogo wanachopewa hakiwafikii huko sasa wanatafuta jinsi ya kusipeleka kwao. Mbona hawawasaidii hao watoto wa mitaani kwanza ndio waje waseme hivi. Yaani ni radhi mtoto afe kuliko kusaidiwa...

Mbele said...

Kwa miaka mingi, nilikuwa nadhani ni jambo jema kuwasaidia fedha watoto wanaoombaomba mitaani. Sikuwa na wazo zaidi, kwani niliona huu ni ukweli mtupu na ubinadamu.

Lakini miaka kadhaa iliyopita, kampuni ya Thomson Safaris ambayo makao yake makuu ni hapa Marekani, iliniomba nisaidie kuongoa kundi la watalii yapata arobaini katika safari ya Tanzania.

Tulipokuwa katika msafara nchini, kiongozi wetu m-Tanzania alituambia kuwa tusitoe fedha wala vitu vingine kwa watoto wanaosimama mabarabarani wakingojea watalii.

Alisema kuwa watoto hao wanashawishika kuacha kwenda shule ili wawepo barabarani. Kwa maana nyingine, kuwapa vitu watoto hao tunahujumu elimu yao. Basi, siku hiyo nilipata angalau wazo jipya kuhusu suala hilo.

Sasa ninajua kuwa ni suala tata, tofauti na pale mwanzo.

Simon Kitururu said...

Kunakipindi nilikuwa nafikiri ni swala tata mpaka nilipostukia institusheni zetu za rushwa ambazo huwa wakaao MAOFISINI wadaio usiwasaidie watu mtaani zimfanyavyo MWENYE N.G.O bongo kuwa na tabia kama serikali ya TANZANIA ambayo inaweza kukudai kodi ila barabara ya kijijini kwakoisifikirie!

Mie kama na mshiko mtoto ntampa mbele ya tangazo kwa kuwa sana sana si kosa lake hata kama yuko mtaani kwa kutumwa labda zaidi ya kutoa kodi ambayo chazaidi najua wenye uhakika hata kwa kugombea ni wabunge ambao zaidi ya kulala sijaona MDINDO!:-(

Nawaza tu kwa sauti!:-(

Anonymous said...

Mimi nasema hiyo ni sababu ndogo sana ya kusema mtoto hatakwenda shule ili akae mtaani aombe. Je wamefanya research waaona hao watoto wanatokea kwenye familia gani mpaka aamue kuomba huko mitaani? Kwa kusema tu hivyo ni wanajaribu kuwaeleza watu wengine kwa juju na kujiosha kuwa wengine wanakataa tu kwenda shule.

Mimi nilikulia Arusha na kule tulikua tunawaita makapurwa. Kutokana na kazi ya baba yangu wakati mwingine mama alikua anapika chakula halafu tunawaita wanakuja kula na wengi niliokua nawafahamu mama zao walikua vichaa na wengine walikua hawawajui hata wazazi wao. Sasa hiyo ilikua kipindi cha mwanzoni wa 90 ukilinganisha sasa hivi ukimwi ulivyomaliza wazazi basi utakuta hao 95% hawana baba wala mama. Na wengine wanaomba ili wakalishe wadogo zao nyumbani. Sasa je ustawi wa jamii umewafuatilia vipi na kujua kuwa hawa watoto kweli wanaweza kwenda shule lakini hawataki?

Kuna shule yeyote iliyoorodhesha wanafunzi ikaonyesha hawa walikua shuleni lakini wameacha na sasa wako mitaani wanaomba?

Let's be serious. Kama hao waliotoa hili tangazo wangeonyesha ni jinsi gani kwanza wanawasaidia hao watoto wa mitaani basi ningewaelewa wakisema pelekeni mahali fulani ambako wanapikiwa na kula hata mlo mmjoja kwa siku la sivyo bado sitawaelewa.

Mbele said...

Anonymous wa tarehe 14, masuali yako ni mazuri na yanachangia kuthibitisha kuwa hili suala ni tata. Nakubaliana nawe kuwa hatimaye unahitajika utafiti makini, ili tulijue suala hili ipasavyo.

Simon Kitururu said...

Hivi si wakati kuna utata wa kuwa kuna MUNGU na SHETANI ,...
... si utata huo haufanyiwi kwa kawaida utafiti hata na wamfagiliao MUNGU?

Nimewaza tu kwa sauti!:-(

Renatus Mgusii said...

Ni kweli suala hili lina utata.Hakuna mpango wowote ulioandaliwa kuhusu watoto hawa. Aidha kama ungekuwepo basi wadau walioandikiwa tangazo hili walipashwa waambiwe kuhusu mbadala wa kuwasaidia watoto hawa. Sipendi sana tabia ya ubinafsi ya watu wetu hasa viongozi. Ni kweli hata NGO zetu sasa ni matatizo wanapata fedha na vifaa vya msaada lakini hata taarifa za matumizi hazipo wazi.Nilishangaa na kusikitika siku moja kuambiwa kuwa kuna shule maaru sana hapa Dar na mikoa mingine inayoendeshwa na Mchungaji maarufu na mwanasiasa ambalo niliambiwa ukitaka mtoto wako anaweza kuandikishwa kama yatima baada ya kutoa rushwa ili kupata nafuu ya ada katika shule hiyo! Nilichoka

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...