Thursday, June 16, 2011

Shughuli ya Waandishi Imefana Minneapolis

Kama ilivyotangazwa kabla, waandishi wa-Marekani Weusi walijumuika katika duka la vitabu la Magers & Quinn Minneapolis. Nilijumuika nao, ingawa mimi si m-Marekani. Tunaonekana pichani kushoto. (Picha ni ya Magers & Quinn Booksellers)


Hii ilikuwa ni fursa ya waandishi kuonesha vitabu vyao na kuongea na wadau na wasomaji, ambao walihudhuria kwa wingi.








Shughuli hii ilitangazwa kama ya waandishi waMarekani weusi. Nilijionea mshikamano mkubwa baina yao na jumuia ya waMarekani weusi. Walifurika duka hili kubwa.







Walikuja watu wazima, vijana, na watoto. Na wote walikuwa na shauku ya kujionea vitabu, kuvipitia na kuvinunua.






Waandishi tulikuwa na kazi kubwa ya kuongea na hao wadau na kujibu masuali yao. Lakini hayo ndio mategemeo ya kila mwandishi.
































































































Huyu dada alisogea kwenye meza yangu, akajitambulisha kuwa mama yake ni m-Mtanzania. Ilikuwa ni ajabu. Wa-Tanzania tuliosoma katika Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison, miaka thelathini na kitu iliyopita tulifahamiana na huyu mama yake. Tulifurahi kukumbushana historia hii.

3 comments:

emu-three said...

Na kweli ilifana, safi sana vitu kama hivyo vikawepo hata huku kwetu nyumbani, waandishi wakutane, hata kupata nafasi ya kutangaza vitabu vyao iitwe siku ya vitabu Tanzania!

Mbele said...

emu-three, shukrani kwa ujumbe. Maonesho ya vitabu yanafanyika Tanzania, nami nimeshuhudia, ila wa-Tanzania kwa ujumla hawahudhurii, labda watoto wa shule. Hata hapa maeneo ya katikati Marekani, nimehudhuria kwa miaka, kama ninavyothibitisha katika blogu zangu. Utawaona wa-Afrika wengine, kutoka nchi kama Kenya, Somalia, Ethiopia, Uganda, Congo, Nigeria, Ghana, na Liberia, lakini sio Tanzania, wala watoto wao.

Katika maonesho niliyoelezea hapa, niliongea na mama mmoja kutoka Congo, nikamwambia kuwa nasikitika siwaoni wa-Tanzania. Alicheka kidogo akasema wanapatikana Blue Nile. Blue Nile ni baa maarufu mjini Minneapolis, ambapo bendi hutumbuiza.

emu-three said...

Inasikitisha kwa kweli Profesa, maana inavyoonekana sisi Watanzania tunasifiwa kwa `starehe'...Ni kweli lakini, watu hawajibidishii kusoma Vitabu, hili tunaliona hapa.
Nakumbuka wakati mmoja nilikuwa nafanya kazi kwenye kampuni ya kuchapa vitabu, wanunuzi wa vitabu walipokuwa wakija pale kwetu walikuwa wakidai kuwa vitabu vyeti ni vikubwa sana...nikawaza kama ni vikubwa ndio vyema maana vitakuwa na mambo mengi.....!
Kwakweli inasikitisha sana! Angalia hata kwenye blogs, tunajitahidi kuandika kwa kupitia njia hii, kwa bure kabisa, lakini angalia iadai ya wasomaji Wakitanzania, na hebu jaribu kuweka picha za vichekesho, starehe, burudani za....utaona utakavyopata wasomaji wengi!

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...