Tuesday, July 18, 2017

Mhadhiri wa Algeria Amekifurahia Kitabu

Mimi kama mwandishi, ninaguswa na maoni ya wasomaji. Leo nimepata ujumbe kutoka kwa mhadhiri wa chuo kikuu kimoja cha Algeria, Samir, ambaye tumewasiliana kwa miaka michache, na nilimpelekea nakala ya kijitabu changu, Notes on Achebe's Things Fall Apart.

Nanukuu sehemu ya ujumbe wake:

I hope this finds you safe. I am so pleased to let you know that your book on Achebe's TFA is very helpful!! It really helped me. It is a pleasure also to inform you that I am citing you in my phd thesis on Gender in Ngugi's fiction. Your name will also be cited in my Acknowledgements and Dedications. Thank you so much....We love you much.

Kwa wale wasiojua ki-Ingereza, napenda kuelezea anachosema mhadhiri huyu kwa ujumla. Anasema kuwa anategemea ujumbe wake utanifikia nikiwa salama. Amefurahi sana kunifahamisha kuwa kitabu changu kuhusu riwaya ya Achebe ya Things Fall Apart ni mchango mkubwa sana na kimemsaidia sana. Anafurahi kunifahamisha vile vile kuwa ananukuu kitabu changu katika tasnifu yake ya uzamifu kuhusu jinsia katika riwaya za Ngugi wa Thiong'o. Jina langu litatajwa katika orodha ya watu waliochangia tasnifu hii. Anahitimisha kwa kusema, "Asante sana....Tunakupenda sana."

Ujumbe wowote kutoka kwa wasomaji makini una manufaa kwangu kama mwandishi. Ninayachukulia maanani maoni yao, hasa nikijua kuwa wametumia hela zao kununua kitabu changu. Kuna wengine ambao ninakuwa nimewapa nakala ya bure. Hao wanaponiandikia maoni yao juu ya kitabu ninaona kama wamelipa fadhila. Maoni yao ni muhimu kwangu kuliko hela.

Kitabu hiki na vingine vinapatikana hapa

7 comments:

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Ndugu Mbele una haki na kila sababu ya kufurahia kupata mwangwi wa msomaji wako. Hata nami nangoja kusikia mwangwi wako juu ya vitabu viwili vya ushairi Kiingereza nilivyokutumia hasa nikizingatia kuwa wewe ni gwiji la Kiingereza na rafiki yangu ambaya hataogopa kunikosoa atakapogundua makosa. Mie si kama Magufuli wala Mkapa wanaoogopa kukosolewa na Mkapa kuwaita wakosoaji wa Magufuli wapumbavu wakati mpumbavu anajulikana kuwa aliwauza watu wake naye akajiuza.

Mbele said...

Shukrani, ndugu Mhango, kwa ujumbe wako. Nami siwaelewi watu wasiotambua na kuthamini unuhimu wa kuhoji na kukosoa, kukosolewa na kukosoana, na pia kujikosoa. Kuhusu vitabu vyako, nilichofanya, kama hatua ya kwanza, ilikuwa kuandika kwenye blogu yako kushukuru kwa kuniletea. Tena hiyo si mara ya kwanza kwako kufanya hivyo. Umeitajirisha maktaba yangu. Kitakachofuata ni hiyo hatua ya kusema neno juu ya tungo zako. Nakutakia kila la heri.

Unknown said...

Hongera sana mzee.

Unknown said...

Kaka habari, hata mi ushairi wa kizungu ndo fan yangu, ndio sababu ya kuwa hapa NMHU kimasomo. Ningependa kuijua blog na mawasiliano yako pia. Ninataka mwakan niungane na prof. Mbele kwenye lile tamasha la Ronchester, kama sijakosea hata kwa kitabu kimoja tu cha ushairi kwa kuanzia. Thanks!

Unknown said...

Mzee ninajipanga mwakan tuwe wote kwenye lile tamasha la ronchester, nikiwa na vitabu au kitaab! Muda ukiwadia tutawasiliana. Thanks!

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

@Daudi Mhengela,
Habari ni nzuri sana. Nimefurahi kukufahamu kupitia uga huu wa ndugu Mbele. Blog yangu ni mpayukaji@blogspot.com wee google Nkwazi Nkuzi Mhango utaona vitabu na machapisho yangu mengi yawe ya kitaaluma au mashairi na makala kwenye magazeti. Ukigoogle jina langu utapata kila kitu. Karibu sana.

Mbele said...

Juzi nilimwandikia mhadhiri Samir kumshukuru kwa ujumbe wake kuhusu kijitabu changu, nikamwambia kuwa kijitabu hiki kinapendwa na wengine kama anavyokipenda yeye, nikampa mfano wa chuo kikuu cha Cornell ambacho, mwaka 2005 walipoamua kuwa wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza wasome riwaya ya "Things Fall Apart," walikiteua kijitabu changu kama mwongozo

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...