Tuesday, September 21, 2010

Kiboko ya Wachawi

Nilipokuwa Tanzania mwaka huu, nilipata wazo la kupiga picha za matangazo mbali mbali ya waganga wa kienyeji, ambayo ni mengi kwenye miji kama Dar es Salaam. Matangazo hayo yanahusu uponyaji wa magonjwa na matatizo mengine ya afya, mafanikio ya biashara na maisha, kuwavuta wapenzi, na kadhalika.

Tangazo hili la "Kiboko ya Wachawi" nililiona Kibamba, kandokando ya barabara itokayo Dar es Salaam kwenda Morogoro, tarehe 28 Julai. Nilipita hapo na walimu wengine watatu kutoka Marekani, kutembelea shule ya sekondari ya Shulua ambayo iko maeneo hayo.

2 comments:

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Da! Prof, hivi hakuna kiboko ya wachawi hapa Tanzania mpaka tu-import kutoka Nigeria?

Uchawi upo kweli ama ni nini?

Simon Kitururu said...

@Mkuu CHACHA : Kweli unashangaa hilo ?


Nakumbuka nilishawahi kwenda kijiji kimoja katika kufanya utafiti fulani/KURIPOTI kuhusu miradi fulani ambayo kinamna NILIHUSIKA, nikafanya kosa la kwenda na rafiki yangu tu kutoka ulaya ambaye alikuwa mtalii tu na wala hahusiki na nachofanya. Bado kidogo watu wakatae kunisikiliza kwa kudhani nambania mgeni kuongea kwa kuwa waliamini miesijui kitu na ajuaye ni huyo Mzungu ila kunaulaji naubania ndio maana kila kitu nafanya mimi.Ilichukua muda kuweka sawa kuwa huyo MGENI ni rafiki yangu tu na hahusiki na nachofanya ili kusikilizwa.

Kunakasumba sehemu nyingi bongo nafikiri tokea enzi za UKOLONI kwa watu kudhani wageni ni zaidi kinamna katika mambo mengi tu.

Naamini ni mpaka katika BIDHAA kuna wengi huamini vya kutoka nchi za kigeni ni bomba zaidi kuliko vya bongo.:-(

Halafu siku hizi na umaarufu wa sinema za Kinigeria ambazo zinastori za kichawi sana tu basi ukijifanya Mnigeria nafikiri moja kwa moja watu hudhani wewe ni profesa wa mambo ya uchawi.:-(

Mwisho: Uchawi upo na umenukuliwa kwa miaka melfu mpaka kwenye BIBLIA.

Tatizo Africa wachawi huficha uchawi ila si ajabu kukutana na mtu ulaya au marekani ambaye hata kwenye facebook page yake akakuambia yeye ni Mchawi.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...