Sunday, October 23, 2011

Taswira za Mjini Songea

Nchi yetu ya Tanzania ni kubwa sana. Ina mikoa, wilaya na vijiji vingi, na siamini kama yuko m-Tanzania atakayeweza kupita kila sehemu. Mimi mwenyewe nimebahatika kutembelea sehemu nyingi katika mikoa mbali mbali. Hata hivyo, kuna sehemu ambazo sijafika, kama vile Bukoba, Mpanda, Sumbawanga, na Singida.

Kutokana na ukweli huo, ninawashukuru wanablogu ambao wamekuwa mstari wa mbele kutuletea habari na taarifa za sehemu mbali mbali za nchi yetu. Blogu ya Mwenyekiti Mjengwa ilinigusa kwa namna ya pekee tangu mwanzo, kwa jinsi alivyokuwa anatembelea vijiji ambavyo wengi wetu hatutavifikia. Kutokana na jinsi nilivyofaidika na jambo hilo, nami najaribu kuleta picha za sehemu mbali mbali, ili wa-Tanzania wengine wapate kuzifahamu sehemu ambako nimefika.

Leo naleta baadhi ya picha nilizopiga mjini Songea mwaka huu. Nimeshaleta taarifa kadhaa za Songea katika blogu hii, kama vile hii hapa. Napangia kuleta taarifa na picha zaidi. Wale ambao hawajafika Songea watapata fununu kidogo kuhusu mahali hapo, ingawa picha zote ni za sehemu ya katikati ya mji.













3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante sana hata kama najua sana Songea lakini nyumbani ni nyumbani nimefarijika sana nimejikuta kama nipo Songea...

Mbele said...

Safari ijayo, panapo majaliwa, nitazungukia sehemu zingine za mji wa Songea, nipige picha. Nina hamu ya kwenda Matogoro, kwa mfano, kwenye kanisa na chuo cha waalimu.

Yasinta Ngonyani said...

Huwa kila mwaka niwapo Songea lazima nifike Matogoro lakini mwaka huu muda ulibana sana.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...