Thursday, November 10, 2011

Maktaba Kuu ya Taifa, Dar es Salaam

Sijui ni wangapi kati ya mamilioni ya watu wanaoishi Dar es Salaam ambao wameingia katika Maktaba Kuu ya Taifa, au wana mazoea ya kuingia humo. Hapa siongelei wanafunzi, kwani hao wanaingia humo. Naongelea watu wasio wanafunzi.

Yawezekana wako ambao wana vijiwe vyao hapa nje ya maktaba, ambavyo wanahudhuria kila siku au kila wiki, lakini hawajawahi kukanyaga ndani ya maktaba hii.

Lakini, Mwalimu Nyerere alipofungua maktaba hii, tarehe 9 Desemba, 1967, alitoa ushauri wa maana, na baadhi ya maneno yake ni haya:

I am also forced to say that we shall probably not be able to go ahead as quickly as we would like, because even when a library service is run with the utmost economy, it still costs quite a lot of money. For a public library should not just be a place where books can be borrowed. It must also be a center for much wider adult education work of all kinds – ranging from the promotion of the desire for literacy by story telling and discussion, to the erudite lectures of visiting professors in our country. The libraries also have an important role to play in overcoming one of their own limitations; for a good librarian backed by a good library, can encourage people to write books as well as read them. Our traditional stories and histories can be written in Swahili so that the whole nation can read them; personal experiences, which are of wider interest, can be written as a story or a book; knowledge gained through practical development work can be written down so that it is shared. (…) (W)e can make our libraries into real cultural and community centers. It is up to us to provide them, to help them develop, and to use them to the full.

(Source: The Mwalimu Nyerere Foundation)

Hebu nijaribu kuyatafsiri kwa ki-Swahili:

Vile vile nalazimika kusema kuwa huenda hatutafanikiwa kusonga mbele kwa kasi ambayo tungependa, kwa sababu hata pale maktaba inapoendeshwa kwa umakini kabisa kimatumizi, bado inagharimu hela nyingi sana. Kwani maktaba ya umma isiwe tu mahali pa kuazimia vitabu. Sherti pawe pia mahali pa kutekelezea suala zima la elimu ya watu wazima kwa mapana yake--kuanzia kuhimiza kusoma na kuandika kupitia usimuliaji wa hadithi na uchambuzi wake, hadi mihadhara ya kisomi ya wahadhiri na maprofesa nchini mwetu. Maktaba pia zina wajibu muhimu wa kuchangia katika kurekebisha mapungufu yanayozikabili; kwani mkutubi bora awapo na maktaba bora, anaweza kuwahimiza watu kuandika vitabu sambamba na kuvisoma. Hadithi zetu za jadi na historia zinaweza kuandikwa kwa ki-Swahili ili Taifa zima liweze kuzisoma; taarifa za uzoefu wa watu binafsi, ambazo ni muhimu kwa jamii, zinaweza kuandikwa kama simulizi au kitabu; ujuzi upatikanao katika shughuli za maendeleo unaweza kuandikwa ili na wengine waupate. (...) (Tu)naweza kuzifanya maktaba zetu sehemu halisi za kuendeshea shughuli za kitamaduni na kijamii. Ni juu yetu kuzifanya ziwepo, kuchangia ustawi wake, na kuzitumia kikamilifu kabisa.

13 comments:

Simon Kitururu said...

Tatizo MAKTABA hakuna BAA na BAA vitabu hakuna na vikiwepo hutumika kama toileti pepa/Makokoneo!:-(

Mbele said...

Kuna mtu anatafuta sehemu ya kuanzishia baa Dar es Salaam, na ameamua kuwa pamoja na ulabu, atakuwa anauza vitabu vyangu humo baa.

Kama unavyojua, walevi wa Bongo wakishapakia ulabu wanapenda sana kutema ung'eng'e ili kuonyeshana nani kasoma zaidi. Inategemewa kuwa vikiwepo hivi vitabu, wataringiana kwa ung'eng'e nani kavisoma :-)

Nitakubipu atakapokamilisha :-)

Simon Kitururu said...

Kuhusu UNG'ENG'E kwenye ULABUB,...


-Umenikumbusha safari yangu iliyopita Bongo nilijikuta nimegongana na MFINI mmoja kwenye Baa moja pale DAR. Sasa tukaanza kuongea Kifini.Haikuchukua muda nikastukia jamaa waliokuwa karibu wakibishana tunaongea lugha gani. Cha ajabu wakahitimisha tunaongea KIINGEREZA ila ni kile Kiingereza kigumu sana ndio maana hawaelewi!:-)

Na chakusikitisha hao jamaa ni Wasomi kabisaa kutokana na shule zao na wafanyiapo kazi!:-(


Ila nasubiria unibipu ishu ikitimilika na lazima ntajitahidi kukatizia hapo .

Mbele said...

Lo, huo ubishi wa walevi na hitimisho lao kuwa walikuwa wanasikia ung'eng'e uliotukuka vimeniacha hoi :-)

Simon Kitururu said...

Kwa bahati mbaya TZ bado kuna watu waaminio kila MZUNGU anajua KIINGEREZA au anaongea Kiingereza!:-(

Mbele said...

Hiyo ni kweli, nami inanikasirisha sana. Nawakuta wazungu Tanzania ambao wanaongea kiIngereza ovyo, lakini waTanzania wanawatetemekea kama vile wanaongea kiIngereza ipasavyo.

Kwa sababu hiyo hiyo, inakuwa vigumu kwa wa-Tanzania hao kuamini kuwa mimi m-Matengo nawafundisha wazungu ki-Ingereza kwenye kiwango cha chuo kikuu hapa Marekani.

Yaani mtu unapokumbana na fikra hizi za wa-Tanzania unatamani kumshika mmoja shati na kumlamba vichwa :-)

Anonymous said...

nimeifurahia mada ya maktaba ila nasikitika wadau wa haari mmekuja a conclusion ya bar jamani tutafute mbinu ili watu wapende kuitumia binafsi imenisaidia nilipata darasa la kunifunza kutumia computer na mtandao bure pale maktaba kuu dar na program inaendelea hadi leo

Anonymous said...

hahahahaaaaaaaaaaaaaa vizuri wadau ila asikwambie mtu maktaba raha jamani sio tu kwa watu wazima na wanafunzi tu pia unaweza kumleta mtoto wako hata wa shule ya awali katika maktaba kuu ya taifa ambapo wana kitengo chao maalum kinachoitwa multimedia ambapo kuna vitu special kwa ajili yao,daah!! karibuni sana wapendwa

mkutubi said...

duh!! kweli watanzania tuna uelewa mdogo saaana bna Maktaba ndo maana hata mjadala umeishia na neno au mtazamo BAA, Maktaba ni eneo mojawapo muhimu saana kwa maendeleo ya ntu buinafsi, na taifa kwa ujumla, humsaidia mtu kuupanua uelewa na akili yake kwa kutumia vyema vitabu, mtandao na kompyuta awapo maktaba.

tujenge tabia ya kujisomea kwa kwenda Maktaba maana kuna eneo zzur na tulivu sana kwa ajili ya kujisomea....tuna muda mwingi saana wa kujisome basi tuuu tunapenda kelele nyingi na kubishania yasiyo ya maana na yasioadd tiji mkwetu. tenga muda wa maktaba kama unavotenga muda wa BAA.

Fadhy Mtanga said...

Siju kwa nini nilipitwa na bandiko hili. Ahsante sana Prof.

Mbele said...

Shukrani nawe, ndugu Fadhy Manga. Blogu zipo nyingi, na wote tunashindwa kufuatilia kila kitu. Ila nashukuru umepita hapa kwangu.

Unknown said...

hapo maktaba wanatoa ISBN?,nilikuwa nahitaji mimi mwandishi wa vitabu.Na gharama yake inakuaje?.

Anonymous said...

Naomba kupata mawasiliano na wahusika wa maktaba kuu naitaji kusajiri kitabu changu kikanuni na taratibu za taifa. Jina language Hamimu Mohammed balongo. Sim number is +255762062995

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...