Friday, April 8, 2011

Nasoma Vitabu vya Dini Mbali Mbali

Kati ya mambo ya manufaa kabisa maishani ni kujielimisha. Nami husoma vitabu kila siku kama njia mojawapo ya kujielimisha. Pamoja na vitabu vya taaluma mbali mbali, hadithi, mashairi, na kadhalika, hupenda kusoma vitabu vya dini.

Nina vitabu vya dini mbali mbali, hasa u-Hindu, u-Islam, na u-Kristu. Nina vitabu kama vile Bhagavad-Gita, Upanishads, Quran, na Biblia. Nina vitabu kuhusu watu muhimu wa dini hizo, kama vile Yesu Kristu, Muhammad na Swami Vivekananda. Vyote hivyo ninavipitia, angalau mara moja moja.

Mimi ni m-Katoliki; habari ndio hiyo. Kwa msingi wa dini yangu, nawajibika kuwajali na kuwapenda wanadamu wote. Yesu alifafanua amri kuu kuliko zote kuwa ni kumpenda Mungu kwa uwezo wetu wote, akili yetu yote, na nafsi yetu yote; kumpenda jirani yetu vile vile, na kuwapenda maadui zetu vile vile. Huu ndio mtihani aliotuachia Yesu.

Sasa kwa vile ukweli ndio huo, ninajiuliza ni njia ipi ya kufuata ili niweze kufaulu mtihani huo. Nimeamua kuwa ni wajibu kujielimisha: kuwafahamu wanadamu, maisha yao, fikra zao, na imani zao. Ni wajibu kuzifahamu dini zao. Naamini tungechangia kujenga mahusiano mema duniani iwapo tungekuwa na utamaduni huu wa kuviheshimu na kuvisoma vitabu vya dini zetu na vile vya dini za wenzetu. Ni muhimu vile vile kusoma vitabu vya wale wasioamini dini, na kuwaheshimu.

4 comments:

Simon Kitururu said...

Uliposema tu wewe ni MKATOLIKI sijui kwanini nikafikiria ni jinsi gani Prisi WILLIAM wa UINGEREZA ni jinsi gani kabla ya kuzaliwa alitakiwa kuukana UKATOLIKI na mpaka ingebidi asimuoe huyo KATE atakaye kumuoa na abakie PRINCE kama huyo KATE angekuwa MKATOLIKI!

Nawaza tu kwa sauti!:-(

Mbele said...

Mimi mwenyewe pia huwa nawaza na kuwazua kuhusu hili suala la kujitaja kuwa ni m-Katoliki.

Siku zilizopita, nilikuwa sioni sababu ya kufanya hivyo. Lakini siku hizi, wamezuka watu ambao wanaelekeza mashambulizi kwa wa-Katoliki na u-Katoliki.

Hapo nami nimeona umuhimu wa kujitambulisha kuwa ni m-Katoliki, ili wapate fursa ya kuniona vizuri, pia watambue kuwa ninaamini ninachoamini, na kwamba maadam jitihada yangu ni kujichunguza nafsi yangu, ufahamu wangu, na matendo yangu ili niimarike katika u-Katoliki wangu, siyumbishwi na hao watu. Kuna ule usemi kuwa kelele za chura hazimzuii ng'ombe kunywa maji.

Simon Kitururu said...

Wakatoliki na WAISLAmu wanatatizo la kudhaniwa kuwa hawajuikufikiria kivyao kwa kuwa kuna wadaio inashuhudiwa ni PAPA au tu SHEKHE aamuaye ambayo wayaletayo kwa jazba mtaani!:-(

Nafikiri UPROTESTANTI ndio moja kitu kihusishwacho mpaka na demokrasia zituangaishazo siku hizi kwa kuwa ndio zilikuja na kuanza kujiuliza na kukosoa mawazo ya wakubwa au tu wale wa aminikao mtazamo wao ufwatwe na wote,.....
atleast ndio kitu nijuacho kifanyacho baadhi ya mambo ya KIKATOLIKI na wadau niwafahamuo waufananishe na UISLAMU kitu kifanyacho maswala yote ya IMANI kuwa banangenge kwa kuwa sijui hata MUISLAMU mmoja afagiliaye imani yenye waendao KANISANI.

Ila mie ni shule ya vidudu ya KIKATOLIKI songea iliyokuwa mbele ya shule ya MAJIMAJI enzi hizo Songea ndio iliyo ni -INTROJUZI kwenye ukatoliki na mpaka sasa hivi sina tatizo nao!

Lakini si nasikia hata akina KENNEDY huko MAREKANi ilikuwa ni tatizo sana kukubalika kwa kuwa ni ukatoliki kwa kuwa inasemekana WENGI waliokimbia ULAYA waanzilishi wa MAREKANI ijulikanayo sasa hivi moja walichokuwa wanakimbia ulaya ni UKATOLIKI?

Anonymous said...

nakupa tano prof.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...